Taarifa kutoka mjini Kano, Kaskazini ya Nigeria, zinasema kuwa watu wengi wamefariki na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la bomu.
Ni baada ya milipuko mitatu inayoaminika kuwa ya mabomu kutokea katika msikiti mkubwa zaidi mjini humoulio katikati mwa jiji karibu na eneo anakoishi Emir au kiongozi wa waisilamu nchini humo Muhammad Sanusi.
Emir huyo kwa sasa yuko nchini Saudi Arabia.
Mabomu hayo yalilipuka wakati maombi ya Ijumaa yalipokuwa yanaendelea.
Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo, alihesabu karibu miili 50 ya waliofariki katika shambulizi hilo.
Taarifa zingine zinasema watu waliokuwa wamjihami waliaingia msikitini humo na kuanza kufyatua risasi baada ya mabomu kulipuka.
Wapiganaji wa Boko Haram, wamekuwa wakifanya mashambulizi katika mji huo ambao ni mkubwa zaidi Kaskazini ya Nigeria.
Mapema mwezi huu , Emir alitoa wito kwa watu kujikinga dhidi ya mashambulizi yanayofanywa na Boko Haram.
Aliwashauri wakazi kujihami na kufanya kila wawezalo kujikinga dhidi ya mashambulizi yanayofanywa na kundi hilo.
Msemaji wa Polisi alisema matamshi ya Emir, yalikuwa ya uchochezi na kwamba watu wanapaswa kumpuuza.
No comments:
Post a Comment