Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kutoka Tanzania, Shy-Rose
Bhanji, ametangaza kusudio la kutaka kuwachukulia hatua za kisheria
wabunge wenzake wanaomshushia tuhuma ambazo amedai zimelenga kumchafua.
Alitoa msimamo huo jana jijini Dar es Salaam wakati akifafanua kuhusiana na tuhuma kadhaa zilizoelekezwa kwake hivi karibuni.
Anatuhumiwa kutoa lugha mbaya kwa baadhi ya wabunge, kuwatukana baadhi ya marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, ulevi wa kupindukia, kufanya fujo na kuvunja chupa ndani ya ndege na kufungwa pingu wakati wa ziara ya wabunge wa EALA nchini Ubelgiji.
Alisema tuhuma hizo ni mkakati wenye ajenda ya siri nyuma yake na kuwa hazina ukweli wowote na kama wanaozusha wana ushahidi waupeleke kwenye ofisi ya Bunge.
“Kwa kuwa tuhuma hizi si tu kuwa ni mbaya kwangu, bali hata kwa nchi yangu, iwapo wabunge hawa watashindwa kuthibitisha madai yao sitosita hata kidogo kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria,” alisema.
Alisema kiini cha shutuma hizo ni kutokana na msimamo wake wa kupinga hatua ya baadhi ya wabunge kutaka kumng’oa Spika wa Bunge hilo, Margaret Zziwa, bila kufuata taratibu zinazotakiwa na kwamba kamwe shutuma hizo hazitamvunja nguvu na ari ya kutetea maslahi ya Tanzania ndani ya bunge hilo. “Ni jambo la kushangaza wabunge kukataa kujadili mambo ya wana-Afrika Mashariki kwa sababu tu ya Shy-Rose Bhanji, haipendezi hata kidogo wabunge kuacha kuzungumzia mambo ya msingi kutaka hadi Shy-Rose achukuliwe hatua kwa kuondolewa kwenye kamati ya Uongozi,” alisema.
Mbunge mwingine wa EALA kutoka Tanzania, Twaha Taslima, alisema kwa kuwa Shy-Rose ni mjumbe wa Kamati ya Uongozi inayosimamia mwongozo wa Bunge hilo kila siku, hivyo kamati hiyo ndiyo ilikuwa na dhamana ya kushughulikia tuhuma za mbunge huyo badala ya kulipeleka bungeni moja kwa moja na kushinikiza achukuliwe hatua.

No comments:
Post a Comment