Saudia yawakataa mayaya wa Uganda - LEKULE

Breaking

27 Nov 2014

Saudia yawakataa mayaya wa Uganda


Mamlaka ya Saudia mjini Kampala imewaonya raia wake nchini Saudia dhidi ya kuwaajiri mayaya kutoka Uganda.

Onyo hilo linajiri baada ya kanda za video za CCTV kumuonyesha Jolly Tumuhiirwe,22,akimtesa mtoto wa miezi 18.

Bwana Haza Al-Otabi ,naibu wa ujumbe wa Saudi Arabia alinukuliwa na gazeti la kiingereza nchini saudi akiwaonya wawanchi wa taifa hilo dhidi kuwaajiri raia wa kigeni kutoka Uganda kuwa mayaya wao wenyewe.

''Uajiri ni sharti ufanyike kupitia makubaliano rasmi''bwana Al-Otaibi alisema.

Harakati ya gazeti la the monitor nchini Uganda kuwasiliana na afisa huyo ziligonga mwamba baada ya kudaiwa kuwa mikutanoni siku nzima.
Inadaiwa kuwa Gazeti hilo la Saudia linasema kuwa bwana Al-Otaibi aliitoa kanda hiyo ya video kwa makusudi kwa kampuni zinazowaajiri wafanyikazi wa nje na ambazo mwezi mmoja uliopita ziliweka makubaliano na wizara ya wafanyikazi nchini Uganda ili kuwaajiri mayaya na madereva.

''Walioajiriwa kutoka Uganda hawatapewaza Viza kuingia nchini Saudia iwapo makubaliano hayo hayatafanyika kwa njia rasmi'',alinukuliwa akisema.

Katika mktaba huo kati ya Uganda na Saudia takriban viza 500 zilitarajiwa kupewa mayaya 400 wa Uganda na madereva 100 kufanya kazi nchini humo.

''Kumekuwa na matatizo na uajiri unaoshirikisha raia wa Uganda nchini Saudi Arabia.

Wengi ya mayaya wa Uganda wanaowasili Saudi Arabia huondoa mda mfupi baadaye na kushindwa kumaliza siku 20 n wafadhili wao'' mjumbe huyo alisema.

Amesema kuwa mayaya hao hulalamika kwa balozi yao kwamba wanahitaji haki zao za kifedha.Lakini Wafadhili wa saudia wanadai kwamba hawawezi kuwalipa kwa kuwa wameshindwa kufanya kazi kwa mwezi mmoja.

Lakini msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni nchini Uganda Fred Opolot ,amesema kuwa ubalozi wa Saudia haujatoa lalama yoyote kuwahusu.

No comments: