Rais Kikwete asema amepona Saratani - LEKULE

Breaking

29 Nov 2014

Rais Kikwete asema amepona Saratani


Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema amepona saratani baada ya kufanyiwa upasuaji mapema mwezi huu nchini Marekani.

Kiongozi huyo wa Tanzania mwenye umri wa miaka 64 ametoa hotuba kwa taifa kuelezea afya yake..

"Niligundulika kuwa na hatua ya pili ya saratani ya kibofu, ambayo baadaye ikaonekana kuwa ni hatua ya kwanza," alisema Kikwete katika hotuba iliyotangazwa moja kwa moja kupitia televisheni akiwa uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam baada ya kurejea kutoka Marekani.

Aliongeza kuwa madaktari wamesema sasa hali yake shwari: "Madaktari walisema saratani haikuenea katika sehemu nyingine za mwili na baada ya upasuaji sasa wamesema nimepona saratani."

Alisema aligundulika kuwa na saratani ya kibofu zaid ya mwaka mmoja uliopita na alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Johns Hopkins Hospital tarehe nane Novemba.

Kikwete ambaye anamaliza muhula wake wa pili mwakani amesema wananchi wajenge tabia ya kupima afya zao ili wagundue maradhi mapema

No comments: