Mwaka mmoja uliopita siku kama ya leo tarehe 21 Novemba lilianza
vuguvugu la maandamano kutaka Ukraine kukaribiana na mataifa ya Ulaya
magharibi katika uwanja maarufu wa Maidan Nesaleschnosti, "Uwanja wa
Uhuru".
Kwa mshangao wa wengi serikali ilizuwia utiaji saini makubaliano ya kukaribiana na Umoja wa Ulaya. Na huo ukawa mwanzo wa maandamano ya umma dhidi ya serikali. Mmojawapo wa waasisi wa vuguvugu hilo ni Mustafa Najem. Maandamano hayo anasema muasisi wa vuguvugu hilo yalitokea bila matayarisho maalum katika uwanja wa Maidan.
Wakati utawala wa zamani wa Ukraine ulipotangaza , kwamba unaondoa hatua ya kutia saini mkataba na Umoja wa Ulaya ghafla ukurasa wa facebook ulijaa taarifa za watu kupinga hatua hiyo. Mimi pamoja na wengine wengi tulikuwa na hakika, kuwa ulikuwa ni mzaha tu
Tulikuwa bado na matumaini , kwamba rais Viktor Janukowitsch atatia saini makubaliano hayo.
Mapinduzi ya rangi ya chungwa
Kiishara wakati huo huo , tarehe 21 Novemba mwaka 2004 ndio siku mapinduzi ya rangi ya chungwa yalipoanza nchini Ukraine.
Ndio sababu tuliwatolea wito watu , kukusanyika katika uwanja wa Maidan. Yalikuwa maandamano , lakini hakukuwa na wito wa mapinduzi.
Wito wangu ulikuwa kuwataka kila mmoja wa marafiki zangu na washirika , achukue hatua katika ukurasa wa facebook.
Hata hivyo wanasiasa hawakuamini , kwamba wananchi watajitokeza. Lakini walijitokeza.
Ilipofika usiku wa manane walikuwapo tayari maelfu ya watu katika uwanja wa Maidan.
Lakini ni kipi kilichofanikiwa na kipi hakikuenda sawa katika mapinduzi hayo ya umma.
Kizazi kipya kimeamua
Mustafa Najem anasema kile muhimu , japo ni kidogo, ni kwamba hatimaye tumeweza kuamua wapi tunataka kwenda. Ukraine imetia saini makubaliano na Umoja wa Ulaya. Ukraine haiwezi tena kwenda katika upande mwingine. Lakini kuzungumzia hali yote jumla nyingine kwa kweli ni mapema mno.
Kwa bahati mbaya matokeo ya vuguvugu la Maidan ni vita. Kila kinachotokea leo hii , ni matokeo ya vita hivi. Nafikiri , Maidan imewavutia wengi , ambao wanavutiwa na vuguvugu hili. Ni matumaini yangu , kwamba watafanikiwa na watafanya kila wanaloweza , ili kutopoteza nguvu hizi, ambazo zilikuwapo miaka iliyopita.
Vuguvugu la maandamano ya uwanja wa Maidan hata hivyo lililazimisha
mabadiliko ya utawala nchini ukraine na limefanikiwa. Pamoja na hayo
lakini maelfu ya watu wamepoteza maisha, je gharama hii ya damu ya watu
haikuwa juu mno., aliulizwa Mustafa Najem.
Amekubali kwa kusema kila wakati yanapopotea maisha ni jambo lisilostahili. Kwa upande mwingine kwangu mimi leo ni wazi , kwamba hatukuwa na njia nyingine katika eneo hili , ila kupambana, na wahanga watapatikana.
Hatungeweza kubakia katika ushawishi wa Urusi na mfumo wake wa madaraka, kama alivyokuwa akiongoza rais wetu Viktor Janukowitsch.
Ni kweli kwamba sehemu ya Ukraine inadhibitiwa na ugaidi. Lakini pia nafikiri, kwamba hilo litaondoka. Iwapo tutafanikiwa kujenga nchi yenye mvuto mzuri, sina shaka , kwamba eneo hilo litarejea kwetu.
Hakuna sherehe za kumbukumbu
Kile watu walinachojiuliza , ni kwamba hakuna sherehe ya mwaka mmoja tangu kuanza kwa vuguvugu la maandamano ya umma. Hili ni jambo muhimu sana.
Hii ni maombolezi pamoja na deni kwa wale waliopoteza maisha, ambapo ni lazima wakati wote tuwaweke mbele.
Sifikiri kwamba nimefanya hivyo peke yangu. Ulikuwa uamuzi wa kizazi kipya. Tunataka kuelekea Ulaya. Tunataka Ukraine itawaliwe vingine. Mwanzoni yalikuwa maandamano ya amani. Kwasababu rais Janukowitsch angweza kuzuwia hilo, haya yote yasingetokea . Si kosa letu , kwamba baadaye watu walipigwa risasi. Halikuwa kosa watu kuingia mitaani na kutoa mawazo yao. Kwa muda wa miaka mitatu Janukowitsch aliiongoza Ukraine rasmi kuelekea Ulaya. Yeyote aliyebadilisha mwelekeo huo , ndio anabeba lawama la kile kinachotokea sasa nchini Ukraine.

No comments:
Post a Comment