Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa
Urusi, Sergei Lavrov, ameyashutumu mataifa ya magharibi kwamba yanataka
kubadilisha serikali ya Urusi kwa kuiwekea nchi hiyo vikwazo vya
kiuchumi, kwa sababu ya mzozo wa Ukraine.
Aliuambia mkutano wa
wataalamu wa mashauri ya nchi za nje mjini Moscow kwamba mataifa ya
magharibi siyo yanataka kuifanya Urusi ibadilishe sera zake kuhusu
Ukraine tu, bali yanataka kubadilisha serikali ya Urusi.Marekani na Umoja wa Ulaya zimeiwekea Urusi vikwazo kadha vya kiuchumi kwa sababu zinaishutumu kuwa inawasaidia wapiganaji wa mashariki mwa Ukraine.
Bwana Lavrov alisema vikwazo hivyo vililenga kuharibu uchumi wa Urusi na kuchochea maandamano.
No comments:
Post a Comment