FLAVIAN MATATA AHUDHURIA MISA YA KUWA KUMBUKA WALIOKUFA KWA AJALI YA MV BUKOBA,AKITOKEA MAREKANI - LEKULE

Breaking

21 May 2014

FLAVIAN MATATA AHUDHURIA MISA YA KUWA KUMBUKA WALIOKUFA KWA AJALI YA MV BUKOBA,AKITOKEA MAREKANI




Flaviana apotezea dola 50,000 kuhudhuria misa ya kumbukumbu ya watu waliopoteza maisha MV Bukoba akiwemo mama yake mzazi




Mwanamitindo wa kimataifa kutoka Tanzania Flaviana Matata amekuja nchini kwa ajili ya kuhudhuria misa ya kumbukumbu ya watu waliofariki katika ajali ya meli ya MV Bukoba akiwemo mama yake mzazi na binamu yake.






Matata ameamua kuacha dili la kazi aliyokuwa akitakiwa kuifanya siku ya kesho, kazi ambayo ingemuingizia dola za kimarekani elfu hamsini.


"kweli mungu ana mitihani unaweza ukawa umekaa hauna kazi lakini pale unapokuwa umepanga kitu, kitu kinatokea, saa ingine nasema ni mitihani Mungu anataka kuona uko strong kiasi gani, kwahiyo kama sasa hivi, nilikuwa nakuja huku ikatokea kazi ya hela nyingi sana, ki ubinaadamu ni ngumu kuiachia, lakini at the end of the day lazima uwe na priority kwenye maisha, so i had to sacrifice that for my mom na kile kilichotokea.

Na ilikuwa ni kazi gani hasa?

Mercedes, nafanya kazi sana na Mercedes lakini ilikuwa ni kazi tofauti kabisa wana project yao ambayo wanaifanya, kwahiyo walikuwa wameniita kwa ajili ya hiyo kazi, wanatengeneza kitabu kikubwa kwa ajili ya Mercedes kwahiyo walikuwa wamenichagua mmoja katika, kwasababu kinatumika kwa muda mrefu kidogo.




For that amount of money kazi yao ulikuwa unatakiwa kuifanya kwa mda gani?




"Ni kazi unai-shoot kwa siku moja, unajua sisi tunalipwa kufatana na mda, siku ulizoshoot kuna day rate halafu kuna usage pia na coverage kwamba ina rushwa kwa muda gani na wapi na wapi, kwahiyo ilikuwa within Marekani"







Tarehe 21 mwezi wa tano itaendelea kukumbukwa kwa ndugu jamaa na marafiki waliopoteza maisha yao katika ajali ya meli ya MV Bukoba iliyotokea mwaka 1996.

Mwanamitindo Flaviana Matata ni moja wa waathirika ambapo alipoteza mama yake mzazi na binamu yake na amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kumbukumbu hizo zinafanyika kila mwaka.

No comments: