Sielewi nitumie neno gani badala ya "FACTOS" lakini itoshe tu kusema kwamba kwenye makala hii ninaposema jambo au mambo naamanisha factors.Kuna mambo ambayo yapo na hayakanishiki japokuwa hayaonekani kwa jicho la kawaida na wala kushikika kwa mwili huu wa damu na nyama.Kutoonekana wala kutoshikika hakutufanyi tuyakane yaliyodhahiri,mfano ni Umoja wa Africa na Muungano wa Afrika.Raisi wa kwanza wa Ghana hayati KWAME NKRUMAH alipigania sana uhuru wa Africa,Umoja wa Africa na Muungano wa Africa.Sidhani katika akili yake Nkrumah alijua utofauti iliyoko kati ya Uhuru wa Waafrica na Uhuru wa Africa.Sina hakika kama alielewa vilicyo tofauti kati ya Umoja wa Waafrica na Umoja wa nchi huru za Africa wala tofauti kati ya Umoja na Muungano.Katika lugha ya Kiingereza zamani hizo lilitumika neno "UNITY".Nkrumah baada ya kujenga hoja sana katika majukwaa mbalimbali yaliyowakutanisha viongozi wa nchi huru hatimaye aligundua kwamba ujumbe wake ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa.Maraisi wenzake hawamsikilizi japokuwa wanamsikia na hawamuelewi ingawa walielewa lugha aliyozungumza.Mwisho Nkrumah aliamua kuandika kitabu kama kumbukumbuku ya wito wake kwa vizazi vya Waafrica vitakavyofuata AFRICA MUST UNITE.Kuna sehemu Nkrumah amenukuliwa akiwasihi viongozi wenzake na kuwatahadharisha akisema kwamba "kama hatutaungana leo hatutakuja kuungana tena badala yake tutabaki kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe tukigombania mipaka au kagambania kujitenga zaidi.Unabii wa Nkrumah ulitimia kwa Nigeria kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe 1967 ya jimbo la Biafra,Somalia kupigana kwa sababu ya jimbo la Ogaden,Ethiopia,Angola,Liberia,Congo,Msumbiji na sasa Sudan.Nkrumah alivutiwa na Muungano wa dola za Marekani United States of America na kwa hiyo akatamani sana Africa nayo iwe kama America yaani tuwe na The United States of Africa.Tuwe na serikali moja raisi mmoja kwa Africa nzima,sarafu moja,jeshi moja na bunge moja.Kwa maono yake Nkrumah kama Africa ingeungana ingekuwa nchi yenye nguvu kijeshi,kiuchumi na kisiasa kwa hiyo isingenyanyasika mblele za walimwengu wengine.Sipendi kuzama kwa undani jinsi Shirika la ujasusi la Marekani (CIA)lilivyoingilia kati na kuhujumu fikra za Nkrumah.Lakini hata leo Africa inanyanyasika mno na waafrica tunateswa na mengi,umaskini,njaa,maradhi na vita vya wenyewe kwa wenyewe.Mtu yeyote alie makini akiuliza sababu halisi ni nini jawabu lake si jepesi kupatikana kwa sababu lipo kisogoni,mwaafrica hata akigeuka huku na huku hawezi kuliona.Africa ni konineti tajiri lakini waafrica ndio tunaoongoza kwa umaskini,je?ni kitendawili gani hicho cha umaskini kuishi ndani ya Africa tajiri kupindukia.Umaskini ndani ya utajiri na utajiri ndani ya umaskini jibu lake liko kisogoni,ni jukumu la kizazi kipya cha waafrica(baada ya kutoweka kizazi cha wapigania uhuru)kuibuka na jawabu la kisayansi.Tusipendelee majibu mepesi kwa majibu magumu.Ipo tofauti kubwa kati ya Africa na Waafrica.Sisi umeitwa waafrica na wageni lakini wenyewe hatujiiti waafricawala hatujitambui kama waafrica.Mimi hujitambulisha kama mwafrica anayetoka pande za Africa Mashariki ninapokuwa Marekani kwa sababu Wamarekani wengi hasa wa kawaida hawaijui Tanzania.Inapotokea kutajia Mmarekani jina la Tanzania bado atakuuliza swali Tanzania iko karibu na Nigeria au Africa kusini?Nina rafiki pale Johannesburg,Wamarekani wanaiona Afrrica kama kijiji kiomja kikubwa chenye rasimali nyingi na watu wasioendelea.Vyombo vya habari vyenye malengo potofu vinapotia mkazo kuonyesha matukio mabaya ya njaa,mauaji ya kinyama kwenye nchi zile za kiafrica zenye vita vya wenyewe kwa wenyewe,ni kama wanahitimisha na kutia mhuri kwa Mmarekani wa kawaida aone na kuamini kwamba Africa ni kijiji kinachokaliwa na watu"primitive".Nndio maana Wamarekani wengi wenye asili ya Africa huona aibu kujitambulisha na Africa kutokana na propaganda chafu dhidi ya Uafrica.Lakini wengine waliotambua hila za weupe dhidi ya weusi,wanamtazamo tofauti wanaiona Africa ni sawa na Maka.Inapotokea mwaafrica kuonwa tofauti na vile alivyo ni jukumu lake Mwaafrica kujivumbua upya na kujiona mwenyewe katika uhalisi wake.Ikitokea mwafrica kujiona kama wengine wanavyomuona hapo lazima liibuke tatizo na madhara yatokanayo na kujiona tofauti na uhalisi wake si halali kuwabebesha wengine.Wale wlioamua kumkamata Mwafrica kama mnyama pori na kumpeleka sokoni ni kwa sababu walimuona tofauti na wao vinginevyo,kama wangemuona sawa na wao wasingethubutu kufanya hivyo.Lawama inabidi zimuangukie mwafrica mwenyewe ni kwa nini alikubali kujiona kama wengine walivyomuona badala ya kujiona kama alivyo.Lawama zaidi ni kwa kizazi cha leo,ni kwa nini waafrica bado wanakumbatia dhambi ile ile iliyowafanya babu zao kuteseka?.Ni lini Mwafrica atakapoachana na dhambi yake ya asili.Wale waliokutanika Berlin mmnamo 1884 na kupitisha Azimio lao la kugawana Africa walifanya vile kutokana na walivyoiona Africa na pia walivyomuona Mwafrica.Kilichowaleta wazungu barani Africa ni dhiki zao na uhitaji wao kamwe hawakuja kuanzisha uhusiano wa kindugu baina ya mzungu na mwafrica.Kilichowaleta ni maslahi na kwa hiyo daima utabaki katika misingi hiyo ya maslahi na manufaa na siyo udugu,urafiki wala upendo na kuhurumiana.Jukumu la kuondoa mabaya katika Africa sio la mzungu wala Mmarekani,bali ni jukumu la mwafrica mwenyewe asipotambua hivyo anatenda dhambi mbele za mungu,naam dhambi inayomfanya kustahili hukumu siku ya kiama.Africa ni ya Waafrica na ipo kwa ajili ya waafrica lakini ukweli huu umepinduliwa na kuwa kinyume chake kwamba Africa ni kwa ajili ya wazungu na wageni wengine.Kwa kuwa ukweli umepinduliwa ndio maana utajiri wa Waafrica haupo kwa ajili ya Waafrica,hauwanufaishi waafrica na badala yake unawaponza.Wazungu waliiivamia Africa na kuikalia tangu karne ya kumi na nane,hili limebaki kuwa suala la kihistoria,kwamba baada ya uvamizi wao walianzisha mifumo mipya kwa Waafrica yaani mifumo ya maisha,mifumo ya elimu,mifumo ya uchumi,sheria na kadhalika.Mifumo hiyo ndiyo iliyomfanya mwafrica kuishi kinyume na uhalisia na huo ndio mwanzo au chimbuko la tofauti ya Africa na waafrica.Baada ya uvamizi tukawa na kitu kipya Dautche ost Africa,Congo Bekgium,British Tanganyika Territory,British Somaliland,Rhodesia,Cameroun,Kwa maneno mengine tukawa na Africa nyingi za bandia,yaani Africa ya Mashariki ya Kidachi,Kongo ya Ubelgili,Somalia ya Kiingereza,Msumbiji/Angola ya Kireno n Africa ya Kifaransa.Jambo hili la Africa kugawanywa katika dola la ulaya na waafrica kugeuzwa katika makabila ya kizungu lilionekana dogo machoni pa Nkrumah,ndio maana alitarajia Africa kuungana ndani ya siku moja ilimradi tu viongozi wakiamua kwa dhati ya mioyo yao.Nkrumah hakuona wala kuelewa kile kilichomtokea mwafrica aliyesoma na asiyesoma tangu Azimio la Berlin 1884 hadi enzi hizo za Uhuru 1950.Sawa na sasa hivi wengi wasivyoona wala kutambua tofauti iliyopo kati ya Africa na Waafrica.Ilitokea hali inayofanana na kile kilinachoelezwa kwenye ujumbe wa injili ya mtume Paulo kwa wayahudi(wamataifa) anaposema "basi mtu akiwa ndani ya kristo YESU amekuwa kiumbe kipya ya kale yamekwisha.Kwenye suala la ukoloni barani Africa ikawa "vice versa" kwamba mwafrica kwa miaka mingi aliyoishi ndani ya mfumo wa ukoloni aligeuzwa kuwa kiumbe kingine kipya.Neno linalostahili ni Subject lakini ili kukidhi dhana nimeamua kutumia neno msukule.Kwa kabila nyingi za Africa msukule,ndondocha au ng`hwintunga ni maneno yanayounganishwa na nguvu za kichawi za kumtoa mtu kutoka daraja la utukufu wake hadi daraja lingine la kudhalilishwa na kutumikishwa.Kwenye jambo hili la uvamizi barani Africa kuna uchawi wa dini na uchawi wa elimu uliompindua mwafrica na kumgeuza kiumbe kipya,lakini sio upya ule unaohubiriwa na mtume Paulo bali ni undondocha wa aina yake.Nkrumah alikaa Marekani kwa miaka 20 kabla ya kurudi Ghana na kuongoza harakati za uhuru,alivutiwa na muungano wa madola ya Marekani na kuihusudu nguvu ya kijeshi,kisiasa aliyoiona Marekani.Akatamani laiti Africa ingekuwa moja,akaona dhahiri kwa utajiri wake wa mali asili kama Africa itaungana dola zake na kupata dola moja,hakuna chochote cha kuizuia isiendelee wala kuizuia isiwe na nguvu.Nkrumah alikuwa na maono ya Africa kuwa Super power namba tatu baada ya USA na USSR.Ambacho hakukiona ni factors au mambo halisi yaliyochochea muungano wa madola ya Marekani hadi kupatikana dola moja ya USA,Marekani haikuwahi kugawanywa na watu wake kugeuzwa kwenye kabila zingine na kutamadunishwa upya ikiwa ni pamoja na kupewa lugha zingine.Lakini kwa waafrica mipaka ilipita kati ya kabila moja na kuwatenganishwa watu na kuwapa hisia mpya za mtu kujiona ni mmasai wa kenya,mjaluo wa kenya ama mkurya wa kenya na mwingine wa Tanganyika.Hisia mpya za utaifa zilikuwa ni kikwazo tosha kukwamisha muungano,mfano ni mvutano uliotokea mara baada ya kuundwa kwa Organization for Africa Unity (OAU)mwezi mei 1963.Nchi zinazozungumza kifaransa yaani FRANCAPHONE zikaunda kundi la CONAKRY,na zile zinazosema kiingereza yaani ANGLOPHONE zikaunda kundi la MONROVIA,hatimae mwafaka ukapatikana kwamba makao makuu ya OAU yasiwe kwa mfaransa(Guinea)wala kwa mwingereza (Liberia)badala yake ikakubaliwa yawe Ethiopia Addis Ababa.Nadhani kama nchi za kireno zingekuwako huenda zingekataa makao makuu ya OAU yawe Angola au Msumbiji.Mvutano ule i dalili kwamba mwafrica alikuwa amepoteza uhalisia wake na kwa hiyo mashindano yalikuwa kati ya uingereza na ufaransa uliokuwamo ndani yao akina Nkwame Nkrumah,Julius Nyerere,Ahmed Seiko Toure,Patrice Lumumba,Leopard Senghor na wengineo.Kama makao makuu tu yaliwafanya kuvutana,ingekuwaje kwa Rais mmoja wa Africa?.Huenda wangevutana pasipo na mwafaka tofauti na Marekani ambayo wazungu walipoivamia kwenye karne ya 15 walichokifanya ni kuua wenyeji (wamaori au wahindi wekundu)na walipowamaliza wakajikuta wana uhitaji wa nguvu kazi,wakaamua wanunue watumwa kutoka Africa.Ukombozi wa mwafrica inabidi uende sambamba na historia yake,ukweli wa kihistoria ukiwekwa kando ni mwanzo wa kupotea njia,maana mtu inampasa ajue kule atokako ndio ajue kule aendako.Tofauti kati ya Africa na Mwafrica ni dhahiri kwamba Africa ni nchi,Africa ni mali zake za asili,hizo ndizo wazungu na wageni wengine wanapigania kufa na kupona,hakunaaliye tayari kuzikosa.Lakini hawana mpango na Mwafrica,hata akifa na kutoweka kama walivyotoweka weusi huko Australia ama Wamaori huko Canda na Marekani hawatajali.Linapokuja suala la uhusiano kati ya Mwafrica na wageni watokao nje ya bara hili ni ule wa hapendwi mtu ila mali yake.Vipi uhusiano wa Mwafrica na Mwafrica mwenzake?,Hapo ndipo kinapoibuka kitendawili cha mifumo aliyoianzisha mkoloni na kuwaridhisha wapigania uhuru wa miaka ya tisini.
1 Apr 2014
New
MAKUBWA ASIYAONA MWAFRIKA YAPO KISOGONI KWAKE.

About SOSTENES LEKULE JR
Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
MAKALA
Tags
MAKALA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment