KEN ASTON MWASISI WA KADI NYEKUNDU NA NJANO KATIKA MCHEZO WA SOKA. - LEKULE

Breaking

2 Apr 2014

KEN ASTON MWASISI WA KADI NYEKUNDU NA NJANO KATIKA MCHEZO WA SOKA.



KEN ASTON
Gordon Strachan. MWAMUZI ALIYEASISI KADI NYEKUNDU,NJANO DIMBANI.
ALITUMIA WAZO LA MATAA YA KUONGOZA MAGARI BARABARANI
ZILITUMIKA RASMI MARA YA KWANZA KOMBE LA DUNIA 1970
Pamoja na umuhimu wake kati historia ya soka,lakini jina la KEN ASTON si maarufu kama wengine akiwemo mfalme wa mchezo huo Edson Arantes Nasciomento-PELE.Japosoka ni mchezo wenye wapenzi na mashabiki wengi zaidi duniani,lakini ukilitaja jina la Ken Aston si wengi wanaoweza kujua kama huyu ni mtu wa aina yake katika mchezo huo.Lakini kutokana na umuhimu wake katika mchezo huo,kurasa za mbele za vitabu vya shirikisho la Soka la Kimataifa(fifa) vimempa heshima nguli huyo kuliko hata raisi wa shirikisho hilo Sepp Blater.

KEN ASTON NI NANI?
Alikuwa ni mwamuzi wa soka wa Kiingereza mwasisi wa wazo la matumizi ya kadi nyekundu na njano katika mchezo wa soka,kwamba kadi ya njano iwe ni onyo kwa mchezaji husika na ile nyekundu kwa kosa kubwa la kumtoa nje.Akisimulia jinsi alivyoupata msukumo huo,Ken anasema ilikuwa ni katika mechi ya robo fainali ya kombe la Duunia la mwaka 1966 nchini Uingereza,Nilimuona mwamuzi mwenzangu Rudolf Keitlin(mjerumani).akipata wakati mgumu kumtoa nje ya uwanja mshambuliaji wa Argentina Antonio Ratin aliyekuwa amemchezea vibaya mchezaji wa England
Anasema kwa vile mwamuzi Rudolf hakuwa akijua Kijerumani pia Rattin hakua akijua Kijerumanui,ikawa ni kituko pale uwanjani kwani maelewano yalikosekana.Hapo ndipo nilipopata wazo la kuwa na ishara ambayo itakuwa wazi na yenye kufahamika kwa wote katika kuondoa usumbufu kama alioupata Rudolf siku ile anasema na kuongeza.Nilitazama pia kazi za taa za kuongoza magari barabarani,kwamba njano jiandae na nyekundu ni kuondoka.Baada ya wazo langu kukubalika,tulizitumia kadi hizo kwa majaribio katika michuano ya soka ya olimpiki ya mwaka 1968.Ken anasema miaka miwili baadae 1970 ndipo yalipoanza matumizi ya kadi hizo kwa mara ya kwanza katika kombe la dunia nchini Mexico na kuanzia mwaka 1982,kadi hizo zikawa rasmi kwa mchezo huo duniani kote.
Kwa upande wa matumizi ya kadi hizo katika michuano a kombe la Dunia fainali iliyowahi kutumia kadi nyingi zaidi nyekundu ni ni mwaka 2006 nchini German.Katika fainal hizo jumla ya kadi nyekundu 30 zilitolewa,fainali za ufaransa mwaka 1998,(23) Korea Kusini na Japapn mwaka 2002 wakifungana na na fainali za 2010 za Afrika Kusini kwa kadi 17.Mechi inayoshikilia rekodi ya kuwa na kadi nyingi nyekundu katika fainali hizo za mwaka 2006 ni Ureno na Uholanzi ambayo ilimalizika huku kadi nne nyekundu na 16 za njano zikitolewa.Rekodi zinaonyesha nyota aliyewahi kulimwa kadi nyekundu mapema zaidi katika ya kombe la dunia ni Jose Batista wa Uruguay katika fainali za mwaka 1986.Nyota huyo alikumbana na kadi nyekundu katika sekunde ya mchezo baada ya kumkwatua kwa nyuma mchezaji wa Scotland



No comments: