UKWELI. - LEKULE

Breaking

31 Mar 2014

UKWELI.













UKWELI
Ukweli hauwi ukweli kwa sababu unakubaliwa na watu wengi bali ukweli ni ukweli kwa sababu ni UKWELI.Kwa sababu hiyo tunaufunua ukweli siyo kwa sababu ya kufurahisha kikundi Fulani na kukisoa kikundi kingine bali tunaufunua ukweli bila kujali na kupendelea kikundi kinachodai kwamba ndicho chenye UKWELI wote.Hatuufunui ukweli kwa lengo la kuwafurahisha baadhi ya watu na kuwadhalilisha watu wengine bali tunaufunua ukweli ili ufahamike kwa watu bila kujali nani yupo kwenye ukweli na nani yuko kwenye makosa.Bahati mbaya baadhi yetu tunafurahi tunapoona makosa yakisemwa kwa watu wengine lakini makosa yakisemwa juu yetu hatupo tayari kukubali kwamba tupo kwenye makosa.Ukweli hauwi ukweli kwa sababu umekubaliwa na kuaminiwa na watu wengi kama ukweli kwa muda mrefu bali ni ukweli ni ukweli hata kama umefunuliwa/unafunuliwa leo kwa lengo la kufunua makosa katika kile kilicho aminiwa kwa muda mrefu kama ni UKWELI.
Tunajua dhahiri kwamba kwa sababu adui wa ukweli yupo kazini kwa lengo la kuupinga ukweli kwa kadri awezavyo ndivyo hatushangai kuona baadhi ya watu wakiungana na adui huyo kwa kuupinga ukweli ulio wazi.Tunajua pia kwamba haiwezekani kwa watu wote kuukubali ukweli kama ulivyo na kama hilo litatokea ni wakati adui wa ukweli atakapoangamizwa na hivyo kutokuwepo kwa mpinzani wa ukweli.Maadam adui wa ukweli angalipo ,tutaendelea kushuhudia wapinzani wa ukweli wakijitokeza waziwazi na kuendelea kuupinga ukweli huku wakidhani kwamba wanautetea ukweli.Ndivyo ilivyotabiriwa kwamba katika siku za mwisho watu wengi watajitenga na imani na kusikiliza mafundisho ya uogo yanayotolewa na mashetani.Watu wengi wataupenda uongo na kuuchukulia ukweli.Wengi wa wapinzani wa ukweli watakwenda mbali zaidi ya kuupinga ukweli na hata kufikia kiwagno cha kuwaua wale wanaufunua ukweli,wakidhani wanamfanyia kazi mungu kamaalivyodhani Yule SAULO enzi za mtume wa kwanza.Hata hivyo tunajua na kuamini kwamba katikati ya wapinzani wa ukweli,wapo watu wanaotafuta ukweli kwa nguvu zao zote na wapo tayari kuupokea na kukubali ukweli wa thamani kubwa kuliko kitu chochote kinachoweza kupatikana duniani na hata mbinguni pia. Watu hao wapo tayari kuachana na makosa yaliyodhaniwa kuwa ni ukweli pindi wanapoonyeshwa makosa yaliyo wazi.Hivyo kwa sababu ya watu hao tunaendelea kuutoa ukweli wote bila ya kujali wala kuogopa upinzani unaoweza kuibuka dhidi ya ukweli na hata dhidi yetu.Tunafanya hivyo tukijua na kuwa na uhakika kwamba mwenye ukweli a anazo nguvu zaidi ya kiumbe chochote na yeye yupo upande wetu kwa sababu nihitaji lake kwamba ukweli ufunuliwe na kuwekwa wazi kwa watu wote kabla hajachukua hatua ya kumuangamiza adui wa ukweli na wote walioshikamana naye kwa kuupinga UKWELI.
Tunapoendelea kufunua ukweli hebu tuwasikilize watu mashuhuri walivyouona ukweli na nguvu zake GEORGE SANTAYA aliwahi kusema hivi HE WHO DOES NOT REMEMBER HISTORY IS CONDEMNED TO REPEAT IT,Hapo alimaanisha kwamba mtu yeyote asiyeikumbuka historia yuko hatiani na anapaswa kurudia kuikumbuka historia,.Ili tupate kuujua ukweli kama ulivyo hatutakiwi kuisahau historia maana bila kujua yaliyopita ni vigumu kujua yaliyopo na yatakayokuwapo.LORD ACTION akasema POWER TENDS TO CORRUPTS ABSOLUTELY;akimaanisha kwamba Ipo nguvu yenye tabia ya kupotosha kwa ukamilifu.Awali nilisema kwamba ukweli hauwi ukweli kwa sababu umeaminika kama ukweli kwa karne nyingi.Lord Action alimaanisha kwamba watu wengi wamepotoshwa na nguvu ya uongo kwa sababu imekuwa kazi kwa muda mrefu zaidi.Pamoja na uwepo wa nguvu yenye tabia ya kupotosha kila mtu anao uhuru wa kuchagua ama kuwa chini ya utawala wa nguvu hiyo au dhidi ya nguvu hiyo.Hapa Wiliam Allen White anasema LIBERTY IS THE ONLY THING YOU CAN HAVE UNLESS YOU ARE WILLING TO GIVE IT TO OTHERS,akimaanisha kwamba Uhuru ndicho kitu pekee mtu anachoweza kuwa nacho isipokuwa kama amechagua kukitoa kwa watu wengine.Lakini je? Ni uhuru wa namna gani?.Ni uhuru wa dhamira.Ukweli ni kwamba nguvu ya upotoshaji haina nguvu kama mtu hajautoa uhuru wake wa dhamira ili uwe chini ya nguvu hiyo.Mtu anaweza kumiliki mali za kila namna lakini hana uhuru wa kumiliki mali hiyo.Wakati wowote hata kama mtu hataki,anaweza kunyang`anywa mali zakelakini hawezi kunyang`wa uhuru wa dhamira kama hajakubali kuutoa uhuru huo kwa hiari yake mwenyewe .Mtu anaweza kunyang`wa uhuru wake wa kuishi lakini kamwe hawezi kunyang`wa uhuru wa dhamira hata kama anakabiliwa na kifo.Wengi wametoa uhuru huo wa dhamira ili uwe chini ya mamlaka za watu wengine.Wanaweza kulazimishwa na mchungaji,padre,sheikh,imamu au na hata papa,kuamini jambo fulani linalohusu hatma ya maisha yao,kwa sababu wameutoa uhuru wao wa dhamira kuwa ni viongozi lakini kumbe ni mbwamwitu wakali waliojipenyeza ndani ya zizi kwa lengo la kuwakamata na kuwala kondoo bila huruma yoyote.



By Sostenes Lekule (tazama)

No comments: