411,127 KATI YA 427,609 KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKANI 2014. - LEKULE

Breaking

28 Dec 2013

411,127 KATI YA 427,609 KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKANI 2014.



kATIBU MKUU oFISI YA waziri mkuu TAMISEMI-Jumanne Sagini akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya wanafunzi 411,127 kati ya 427,609 sawa na asilimia 96.15 waliofaulu mtihani wa darasa la saba 2013 wataanza kidato cha kwanza mwakani 2014.

Kati yao wasichana ni 201,021 na wavulana 210,106 na huku kiwango cha wanafunzi waliochaguliwa mwaka huu wakiwa wameongezeka kwa asilimia 31.37 ikilinganishwa na asilimia 64.78 waliochaguliwa awamu ya kwanza mwaka huu.

Matokeo yanaonyesha kuwa jumla ya wanafunzi 427,609(wavulana 218,093 na wasichana 209,516)walifaulu kwa kupata alama A-C kati yas 844,938 waliofanya mtihani ikiwa ni sawa na asilimia 50.61...takwimu zinaonyesha ongezeko la asilimia 19 la ufaulu ikilinganishwa na asilimia 30.6 mwaka jana.

1 comment:

Unknown said...

kazi ni nzuri ila badlisha background ili maandishi mendine yasomeke