Biogas ni nishati mbadala inayotokana na kinyesi cha Binadamu,ng`ombe na nguruwe,nishati hii ni rahisi kuitengeneza na kuitunza kwa mtu wa kipato cha chini.Nishati hiii ya gas huweza kutumika kwa kupikia kama gas,kuwasha taa na kusukuma mtambo wa generator na ukafua umeme bila tatizo.Nishatii hutmika sana katika mataifa ya China na mataifa mengine ya Asia.
Ni jambo la kusikitisha kwamba Tanzania inayosifiwa kuwa ni nchi ya pili katika kanda ya Afrika Mashariki kuwa na mifugo wengi wa aina ya Ng`ombe,lakini imeshindwa kuwawezesha wananchi wake kuweza kuwapa elimu ya kutosha na kuweza kuwa na mitambo ya biogas.Naamini kuwa serikali kwa kuwatumia wataalamu wachache wa CARMATEC wenye makao makuu yao Arusha wanaweza kuwatumia wataalamu hao kuelimisha jamii ya Watanzania faida ya kuwa na biogas.Itakuwa imemaliza kabisa tatizo la upungufu wa umeme na pia kuwapunguzia Tanesco majungu ya kasambaza umeme wa kawaida kwa watumiaji ambao wanatumia umeme huo kwa matumizi ya kuwasha taa na matumizi mengine madogo madogo.Nimeona hayo kwa baadhi ya wananchi wachache wenye mitambo hiyo ya biogas.Hivyo naweza kusema kuwa TANZANIA BILA MATATIZO YA UMEME INAWEZEKANA KWA KUTUMIA BIOGAS.
27 Dec 2013
New
About SOSTENES LEKULE JR
Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
BURUDANI
Tags
BURUDANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment