Broad Based InterSect Organisation yatangaza tuzo mpya za AMAN - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Wednesday, 27 January 2016

Broad Based InterSect Organisation yatangaza tuzo mpya za AMAN

pic 1
Katibu Mtendaji wa Broad Based Intersect Organization (BBIO) Amani Joram Mgullo (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya utambulisho wa Tuzo mpya za AMAN AWARD katika tasnia ya Muziki, Filamu na Habari. Kushoto ni Afisa Mahusiano Balozi Gepard na kulia ni Afisa Habari Salesi Malusa.
pic 2
Afisa Habari wa Broad Based Intersect Organization (BBIO) Salesi Malusa (Kulia) akitoa ufanunuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) namna ambavyo wananchi watashiriki kuchagua washindi wa tuzo hizo kwa kuwapigia kura. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa (BBIO) Amani Joram.


Taasisi isiyo ya kiserikali “Broad Based Intersect Organization” (BBIO) ambayo inaratibu uhamasishaji na uimarishaji wa mikakati ya maendeleo, yenye makao makuu mjini Dodoma imetambulisha tuzo mpya ziitwazo AMAN Awards katika tasnia za muziki, filamu na habari.
Tuzo hizo zimetambulishwa leo, jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo Aman Joram Mgullo.
Mgullo alisema kuwa, tuzo hizo zimetokana na mradi uitwao “Advocacy Mission Awards Network” (AMAN) unaohusika na uhamasisha na uimarishaji wa juhudi za utekelezaji wa mikakati ya maendeleo
“Wazo la utoaji wa tuzo za AMAN limekuja baada ya Tanzania pamoja na mataifa mengine ulimwenguni kuzindua mkakati mpya wa maendeleo (the Agenda 2030 of Sustainable Development Goals) ikiwa na adhima ya kutengeneza Maisha bora na Dunia bora kwa kila mwanadamu ulimwenguni,” alisema Mgullo.
Mgullo aliongeza kwa kusema kuwa, kutokana na mikakati mingi iliyotangulia kutofanikiwa kufikia malengo yake na kufanya jamii nyingi kuendelea kuishi katika hali duni ndicho kilichopelekea taasisi ya BBIO kufanya juhudi za ushawishi na uwezeshaji kupitia wasanii na wanahabari ili mradi huo wa maendeleo ufikie malengo yake kupitia tuzo za AMAN.
Kutokana na tafiti nyingi kuthibitisha kuwa tasnia za muziki na filamu, kupitia vyombo vya habari zinauwezo mkubwa wa ushawishi na uwezeshaji kwa jamii. Hivyo kwa kuwashilikisha wasanii kutoa ujumbe wa maendeleo kwa jamii kupitia tuzo za AMAN kutaleta mabadiliko kwa jamii ya Tanzania.
Mgulla alizitaja tuzo zitakazowaniwa kuwa ni Aman Music Awards, Aman Film Awards na Aman Media Awards ndani ya kila Tuzo kutakuwa na vipengele tofauti tofauti, na wananchi watashiriki kwa kupigia kura na kuchagua msanii au mwanahabari ambaye amefikisha ujumbe wa maendeleo katika jamii.

Lengo la tuzo za AMAN ni kuhakikisha dhima ya maisha bora na dunia kwa kila mwanadamu kwa kuchochea umahiri katika kutoa, kueneza na kufikisha ujumbe wa maendeleo endelevu kupitia tasnia za muziki, filamu na habari
Post a Comment