Katibu
Mtendaji wa Broad Based Intersect Organization (BBIO) Amani Joram Mgullo
(katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya
utambulisho wa Tuzo mpya za AMAN AWARD katika tasnia ya Muziki, Filamu
na Habari. Kushoto ni Afisa Mahusiano Balozi Gepard na kulia ni Afisa
Habari Salesi Malusa.
Afisa
Habari wa Broad Based Intersect Organization (BBIO) Salesi Malusa
(Kulia) akitoa ufanunuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) namna
ambavyo wananchi watashiriki kuchagua washindi wa tuzo hizo kwa
kuwapigia kura. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa (BBIO) Amani Joram.
Taasisi
isiyo ya kiserikali “Broad Based Intersect Organization” (BBIO) ambayo
inaratibu uhamasishaji na uimarishaji wa mikakati ya maendeleo, yenye
makao makuu mjini Dodoma imetambulisha tuzo mpya ziitwazo AMAN Awards
katika tasnia za muziki, filamu na habari.
Tuzo hizo zimetambulishwa leo, jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo Aman Joram Mgullo.
Mgullo
alisema kuwa, tuzo hizo zimetokana na mradi uitwao “Advocacy Mission
Awards Network” (AMAN) unaohusika na uhamasisha na uimarishaji wa juhudi
za utekelezaji wa mikakati ya maendeleo
“Wazo la
utoaji wa tuzo za AMAN limekuja baada ya Tanzania pamoja na mataifa
mengine ulimwenguni kuzindua mkakati mpya wa maendeleo (the Agenda 2030
of Sustainable Development Goals) ikiwa na adhima ya kutengeneza Maisha
bora na Dunia bora kwa kila mwanadamu ulimwenguni,” alisema Mgullo.
Mgullo
aliongeza kwa kusema kuwa, kutokana na mikakati mingi iliyotangulia
kutofanikiwa kufikia malengo yake na kufanya jamii nyingi kuendelea
kuishi katika hali duni ndicho kilichopelekea taasisi ya BBIO kufanya
juhudi za ushawishi na uwezeshaji kupitia wasanii na wanahabari ili
mradi huo wa maendeleo ufikie malengo yake kupitia tuzo za AMAN.
Kutokana
na tafiti nyingi kuthibitisha kuwa tasnia za muziki na filamu, kupitia
vyombo vya habari zinauwezo mkubwa wa ushawishi na uwezeshaji kwa jamii.
Hivyo kwa kuwashilikisha wasanii kutoa ujumbe wa maendeleo kwa jamii
kupitia tuzo za AMAN kutaleta mabadiliko kwa jamii ya Tanzania.
Mgulla
alizitaja tuzo zitakazowaniwa kuwa ni Aman Music Awards, Aman Film
Awards na Aman Media Awards ndani ya kila Tuzo kutakuwa na vipengele
tofauti tofauti, na wananchi watashiriki kwa kupigia kura na kuchagua
msanii au mwanahabari ambaye amefikisha ujumbe wa maendeleo katika
jamii.
Lengo la
tuzo za AMAN ni kuhakikisha dhima ya maisha bora na dunia kwa kila
mwanadamu kwa kuchochea umahiri katika kutoa, kueneza na kufikisha
ujumbe wa maendeleo endelevu kupitia tasnia za muziki, filamu na habari
No comments:
Post a Comment