Ban aikemea Syria - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Friday, 15 January 2016

Ban aikemea Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema kukosesha watu chakula kutumika kama silaha katika mzozo wa Syria ni uhalifu wa kivita.
Ban Ki Moon amezituhumu pande zote nchini humo kukosa busara kutokana na hatua hiyo.
Ufaransa, Uingereza na Marekani wametoa ombi la kufanyika kwa kikao cha dharura cha Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, kutaka kuondolewa kwa hali hiyo ya kuzingirwa, ambako maelfu ya watu wamekwama na pia kutaka, misaada ifikishwe.
Kamishna wa Shirika hilo la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein amesema wote waliohusika na kuwakalisha watu njaa washtakiwe.BBC
Post a Comment