MKUTANO WA AFRIKA WA USALAMA WA MITANDAO WAFANYIKA DAR ES SALAAM - LEKULE

Breaking

1 Jul 2016

MKUTANO WA AFRIKA WA USALAMA WA MITANDAO WAFANYIKA DAR ES SALAAM


A1
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Dkt. Yahaya Simba akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Afrikawa wa Usalama wa Mtandao katika ufunguzi wa mkutano huo kwa Niaba ya Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
A2
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Oracle System Ltd Janusz Naklicki, akitoa Mada kwenye Mkutano wa Afrika wa Usalama wa Mtandao uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
A3
Msanifu wa Mifumo ya Mtandao kutoka Kampuni Oracle Enterprise Architecture, Alexander Smirnov akiwasilisha Mada kwenye Mkutano wa Afrika wa Usalama wa Mitandao uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
A4
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Afrika wa Usalama wa Mtandao kutoka kutoka nchi mbalimbali wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo wenye lengo la kupata elimu juu ya usalama wa taarifa na mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
A5
Naibu Katbu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Dkt. Yahaya Simba (kushoto) akiwa na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Oracle System Ltd Janusz Naklicki (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara wa Kampuni ya Oracle System Ltd, wakifuatilia Mada kwenye Mkutano wa Afrika wa Usalama wa Mtandao uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
A6
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Dkt. Yahaya Simba, akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu Mkutano wa Afrika wa Usalama wa Mtandao uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
A7
Kaimu Katibu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Clarence Ichwekeleza akitoa ufafanuzi kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Afrika wa Usalama wa Mtandao uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
A8
Baadhi ya Waandishi wa Habari wa kifuatilia mazungumzo ya  Naibu Katbu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Dkt. Yahaya Simba (hayupo pichani) aliyemuwakilisha Waziri  wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa kwenye Mkutano wa Afrika wa Usalama wa Mtandao uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Picha na Hussein Makame-MAELEZO.

No comments: