Mtangazaji wa
Choice Fm cha Dar es Salaam, Jimmy Kabwe (katikati), akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa hafla yakuingia
makubaliano kati ya Timu ya mpira wa miguu ya African Lyon inayoshiriki
ligi kuu Tanzania Bara (Vodacom Premier League) na kituo cha radio cha
Choice FM 102.5, juu ya ushirikiano katika kukuza vipaji na kuboresha
misingi ya uendeshaji wa timu, wengine kushoto kwake alievaa kanzu
ni Mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangezi, na Mkuu wa Vipindi
Choice FM, Antonio Nugaz, Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Choice FM .
Mkuu wa Vipindi Choice FM, Antonio Nugaz (kulia) akitolea ufafanuzi makubaliano hayo ambapo amesema yanalenga kujenga mazingira ya kuweza kutambua na kuvikuza vipaji vya wanamichezo hasa wale wa mpira wa miguu (kushoto), Mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangezi
Amesema
makubaliano hayo yataiwezesha Africani Lyon yenye masikani yake Mbagala
kushirikiana na Choice FM katika kuandaa mashindano na programm
zinginezo ambazo zitaleta mvuto kwa vipaji vya wanamichezo wa Kike na
Kiume.
Mmiliki
wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangezi (katikati), akitoa neno la
shukrani kwa kituo cha radio cha Choice FM 102.5 mara baada ya kuingia
makubaliano .
Mmiliki
wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangezi, na Captain African Lyon, Baraka
Jafari (Nyaka) wakikabidhiwa jezi wakati wa hafla yakuingia makubaliano
kati ya Timu ya mpira wa miguu ya African Lyon inayoshiriki ligi kuu
Tanzania Bara (Vodacom Premier League) na kituo cha radio cha Choice FM
102.5, juu ya ushirikiano katika kukuza vipaji na kuboresha misingi ya
uendeshaji wa timu.
No comments:
Post a Comment