ASKARI
wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kikosi cha 212
kilichopo Milambo mkoani Tabora, ameuawa kwa kipigo kutoka kwa wafugaji
akiwa eneo lake la ujenzi.
Aliyeuawa
katika tukio hilo la juzi katika kijiji cha Usule kata ya Mbugani,
Manispaa ya Tabora ni Crius Mkumozi mwenye umri wa miaka 35.
Mtuhumiwa wa mauaji hayo inadaiwa alikuwa akichunga mifugo kwenye eneo la askari huyo.
Akizungumza
ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Hamisi Issa
alisema askari huyo alipigwa fimbo kichwani na begani baada ya kujaribu
kuondoa ng’ombe waliokuwa kwenye eneo lake.
Kamanda
alisema mtuhumiwa ambaye hakutaka kutaja jina lake, anashikiliwa kwa
mahojiano zaidi na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma za mauaji.
No comments:
Post a Comment