Wakulima
wanapenda kupata ushauri wa kitaalamu ili wapate mafanikio pichani
wakulima wa shahiri wilayani Karatu wakimsikiliza mtaalamu wa kilimo na
mshauri wa TBL Group Dk. Bennie Basson alipowatembelea
Wakulima wanaoshirikiana na TBL wilayani Karatu wakisikiza ushauri wa wataalamu wa kilimo walipotembelewa hivi karibuni
Wataalamu
wa Kilimo kutoka SABmiller Francois Potgieter na Gerhard Greeff
wakikagua mashamba ya wakulima wilayani Karatu walipowatembelea na
kuwapatia ushauri
Zaidi ya
wakulima 700 wa zao la zabibu mkoani Dodoma wananufaika na mpango wa
kilimo shirikishi unaoendeshwa na kampuni ya TDL iliyopo chini ya
kampuni ya TBL Group ambao umeanza kuonesha mafanikio kwa kuwawezesha
wakulima kuongeza uzalishaji katika mashamba yao ya zabibu.
Mkurugenzi
Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin amebainisha hayo wakati akitoa ripoti
ya mwelekeo wa biashara ya kampuni W kwa kipindi cha mwaka ujao ambapo
alisema kuwa mpango shirikishi na wakulima wa zabibu umeanza kutekelezwa
katika vijiji vya Bihawana, Mpunguzi, Mvumi, Hombolo, Mbabala, Veyula,
Makang’wa, Mzakwe na Mbalawala
Alisema
kuwa Chini ya mpango huo wakulima wanawezeshwa kupatiwa utaalamu wa
kilimo kwa kushirikiana na taasisi ya Makutupora Viticulture Training
and Research Center (MVTRC) ambapo mafanikio ya mpango huu yameanza
kuleta mafanikio kwa wakulima kupatiwa elimu ya kilimo cha kisasa cha
zao la zabibu na kuanza kufanya utekelezaji kwa kutumia ushauri wa
wataalamu wa kilimo.
Katika
kuwapatia wakulima motisha wakulima ili wajiunge na waweze kuboresha
maisha yao kupitia kilimo cha zao la zabibu chini ya mpango huu watoto
wa wakulima wa zabibu wamekuwa wakisaidiwa kielimu kupitia mfuko
unaojulikana kama Zabibu na Shule Kwanza
Jarrin
alisema kuwa mpango huu shirikishi tayari umeonyesha mafanikio makubwa
kwa wakulima wa zao la Shahiri katika mikoa ya kanda ya Kaskazini ambao
wengi maisha yao yamebadilika kuwa bora na kuwepo ongezeko kubwa la
ajira kutokana na kilimo cha zao hilo ambalo ni malighafi ya kutengeneza
kinywaji cha bia.
“Kwa
upande wa zao la Shahiri wakulima zaidi ya 3000 wanaendelea
kunufaika.Katika kipindi cha mwaka 2015 mpango huu umewezesha ongezeko
la uzalishaji wa zao hilo kufikia tani 15,574 kiasi ambacho kimevuka
lengo la matumizi na mahitaji ya kampuni”.Alisema.
aliongeza
kuwa kampuni inao mkakati wa kuendelea kufanya kazi na wakulima na
kubadilisha maisha yao kupitia mpango wa kampuni mama ya SABMiller
ujulikanao kama Go Farming ambao tayari umeanza kutekelezwa katika nchi
mbalimbali ambazo imewekeza.
Alisema
lengo kubwa la mpango huu ni kuinua maisha ya wakulima
wadogowadogo,kuongeza kasi ya kukua uchumi na kujenga mfumo mzuri na
endelevu wa kupata malighafi kwa ajili ya viwanda kampuni ya TBL Group
kwa hapa nchini na SABMiller vilivyopo kwenye nchi mbalimbali barani
Afrika
“Mpango
wa Go Farming haulengi kunufaisha wakulima wa Shahiri pekee bali pia wa
mazao mengine kama mtama na mihogo na katika siku za usoni wakulima wa
zao la mahindi watawezeshwa pia na inategemewa hadi kufikia mwaka 2020
zaidi ya wakulima nusu milioni watakuwa wamewezeshwa sehemu mbalimbali
duniani ambako kampuni imewekeza na mamilioni ya wananchi watajipatia
riziki kutokana na kufanya kazi za utekelezaji wake”.
Aliongeza
kuwa matarajio ya mafanikio ya mpango huu katika kipindi cha mwaka 2015
hadi 2020 yanaonyesha kukua kwa asilimia 44 katika nchi 10 ambako
umeanza kutekelezwa na inakadiriwa kuwepo ongezeko la uzalishaji wa
mazao kutoka tani 300,000 kufikia zaidi ya tani 600,000.
No comments:
Post a Comment