Waziri Nnauye akutana na Viongozi wa TAJATI - LEKULE

Breaking

3 Apr 2016

Waziri Nnauye akutana na Viongozi wa TAJATI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipokea zawadi ya kikombe kutoka kwa mtunza fedha wa Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) Bi. Brandy Nelson alipowasili katika ofisi zao kuona shughuli wanazozifanya leo Jijini Mbeya.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisoma kipeperushi alichopewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) ili kuweza kujua kazi wanazozifanya leo Jijini Mbeya alipowatembelea na kuwataka kuendela kuandika habari za kiutafiti ili kuboresha fani ya uandishi wa habari. Kushoto ni mwenyekiti wa TAJATI Bw. Ulimboka Mwakilili na kulia ni makamu mwenyekiti TAJATI Bw. Christopher Nyenyembe.
Mwenyekiti wa TAJATI Bw. Ulimboka Mwakilili (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipotembelea ofisi za TAJATI kuona shughuli wanazozifanya leo Jijini Mbeya.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na viongozi wa TAJATI (hawapo pichani) alipowatembelea ofisini kwao kuona shughuli wanazozifanya leo Jijini Mbeya.
Baadhi ya viongozi wa TAJATI wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) alipofika katika ofisi zao kuona shughuli wanazozifanya na kuwapa motisha wa kuandika habari za kiutafiti leo Jijini Mbeya.
Makamu mwenyekiti TAJATI Bw. Christopher Nyenyembe (kushoto) akimuonyesha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye moja ya ofisi wanayoiandaa kwa ajili ya matumizi ya studio ya kurushia matangazo alipotembelea ofisi zao kuona shughuli wanazozifanya leo Jijini Mbeya.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) baada ya kuzungumza nao leo Jijini Mbeya. 

No comments: