Waziri wa
Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akishukuru kampuni hiyo kwa
msaada ilioutoa kwa watanzania hao wenye ulemavu wa miguu ambapo yeye
ndiye aliyewakabidhi kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kamal Steel, Sameer
Gupta.
Waziri wa
Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akimvisha mguu wa bandia Bw.
Siaga Raphael Kiboko mara baada ya kukabidhiwa kutoka kampuni ya Kamal
Steel ya jijini Dar es salaam kushoto ni Mwenyekiti wa kampuni hiyo Bw.
Gagan Gupta.
Waziri wa
Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza na Bw. Siaga
Raphael Kiboko kabla ya kumkabidhi msaada wake wa viungo bandia vya
mguu.
Mwenyekiti
wa makampuni ya Kama Group , Gagan Gupta wakati wa hafla ilyofanywa na
kampuni hiyo ya Kamal Steel Ltd kiwandani hapo wakati wa utoaji wa
msaada wa viungo bandia, kwa watu wenye ulemavu 16, vyenye thamani ya
zaidi ya sh. milioni 80, hafla hiyo ya kukabidhi msaada huo imefanyika
hivi karibuni jijini Dar es salaam.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR
ES SALAAM)
Waziri wa
Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akiongozana na Bw. Gagan Gupta
ambaye ni mwenyekiti wa kampuni ya Kalam Steel tayari kwa ajili ya
kukabidhi msaada huo.
Waziri wa
Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akifurahia jambo na Bw. Siaga
Raphael Kiboko mara baada ya kumvisha mguu wake huku Mwenyekiti wa
kampuni ya Kamal Steel Bw. Gagan Gupta pamoja na viongozi wengine wa
kampuni hiyo wakishuhudia.
Waziri wa
Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akiongozana na Bw. Joshua
Mwamunyange mara baada ya kumvisha mguu wakena kuanza kujaribu kutembea.
Waziri wa
Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akimbidhi Bi Fatuma mguu wake
wa bandia ikiwa ni msaada kutoka kampuni ya kutengeneza chuma ya Kamal
Steel ya jijini Dar es salaam.
Waziri wa
Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja
na wakuu wa kampuni ya Kamal Steel na baadhi ya walemavu waliokabidhiwa
msaada huo.
Waziri wa
Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akimsikiliza Mwenyekiti wa
kampuni ya Kamal Steel Bw. Gagan Gupta.mara baada ya kukabidhi misaada
hiyo katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Kamal Steel, Sameer Gupta na wakuu
wengine wa vitengo kutoka kampuni hiyo.
KAMPUNI
ya kutengeneza chuma ya Kamal Steel Ltd, imetoa msaada wa viungo bandia,
kwa watu wenye ulemavu 16, vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 80.
Akifunga
kambi ya kutoa viungo bandia hivyo jijini Dar es Salaam sambamba na
kukabidhi vifaa hivyo, Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison
Mwakyembe, alisema, serikali itaendelea kuwawezesha watu wenye ulemavu
nchini ili waweze kukabiliana na changamoto zinazowazunguka ikiwa ni
pamoja na kuwapatia vifaa bandia.
Alisema, suala la ulemevu linagusa maisha ya kila mwanadamu na kwamba mtu yoyote anaweza kufikwa na tatizo hilo.
Alibainisha,
viungo bandia vinauzwa kwa ghalama kubwa ambayo watu wengi wenye
ulemavu hawawezi kumudu kununua hivyo serikali kwa kushirikiana na wadau
wake itaendelea kutoa msaada wa vifaa hivyo.
“Jamii
iamini kuwa wote ni walemavu watarajiwa. Kupoteza kiungo kimoja cha
mwili ni changamoto kubwa. Tunaishukuru kampuni ya Kamal Steel kwa kutoa
misaada hii muhimu ambayo tunaamini kuwa inasaidia kupunguza madhira ya
ulemavu,”alisema Dk. Mwakyembe ambaye kupitia msaada huo ameweza
kuwasaidia watu wenye ulemavu wanne kutoka jimbo lake la Kyela mkoani
Mbeya.
Mwenyekiti
wa makampuni ya Kama Group , Gagan Gupta, alisema,kampuni yake haijatoa
viungo bandia hivyo kama msaada, bali kama wajibu wake kwajamii.
“Tunaamini
kwamba, viungo hivi bandia vitawawezesha kumudu kutembea, kufanya kazi
mbalimbali zitakazo waletea kipato,”alisema Gupta.
Katika
hatua nyingine, Gupta aliahidi kumuajiri mmoja wawatu hao wenye ulemavu
mwenye taaluma ya ufundi mitambo, Siaga Raphael ambapo alisema ajira
yake itaanza leo.
“Huyu
atafundishwa ufundi wa kutengeneza vifaa mbalimbali hasa vya watu wenye
ulemavu hapa, ili aweze kusaidia kuwafundisha watu wenye ulemavu
wengine.Mradi anataaluma hiyo ataanza kazi kesho asubuhi (leo
asubuhi),”alisema Gupta.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kamal Steel, Sameer Gupta, alisema, kampuni hiyo imekuwa mstari
wa mbele katika kusaidia viungo hivyo bandia kwa watu wenye ulemavu
ambapo mpaka sasa imesaidia watu 200.
“Tutaendelea
kuwasaidia kila mara ili tuweze kuisaidiana na serikali yetu
kuwaondolea changamoto wenzetu hawa. Tunaamini wakipewa viungo hivi
bandia wanaweza kushiriki shughuli mbalimbali muhimu zitakazowaingizia kipato,”alisema.
Akizungumza
kwa niaba ya wenzake walio pokea msaada huo, Siaga Raphael, aliipongeza
kampuni hiyo kwa masaada wa vifaa hivyo na kuitaka serikali kuwa
kumbuka watu wenye ulemavu kwa kuwasaidia pia kuwapa taaluma ya ufundi
itakazowawezesha kujimudu kimaisha.
No comments:
Post a Comment