Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maabara za Vetenari Tanzania "TVLA"
Dkt. Furaha Mramba akiwakaribisha baadhi ya wafanyabiashara kutoka
nchini Oman waliopo nchini kwa ziara ya siku tatu (3) inayomalizika leo,
ambao walitembelea katika Taasisi ya utafiti na uchunguzi wa wadudu na
magonjwa waenezayo "VVBDRI -TANGA" inayosimamiwa na wakala hiyo na
kutembelea sekta ya mifugo ili kuweza kujionea fursa za uwekezaji
kupitia miradi hiyo.
Kiongozi
wa ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Oman Bw. Warith Al- Kharusi
akieleza malengo ya ziara yao Mkoani Tanga ambapo alieleza kuwa
wamekuja kutembelea mradi wa shamba la mifugo ili waweze kujionea fursa
za uwekezaji zinazoweza kupatikana kupitia mradi huo na miradi mingine
watakayoitembelea.
Afisa
Mambo ya Nje kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Kikanda na Kimataifa Bw. Hangi Mgaka wa pili kutoka kushoto
ambaye pia aliratibu Ziara hiyo akifuatilia uwasilishaji wa taarifa
kabla ya ziara kuanza.
Ujumbe
wa wafanyabiashara kutoka Omani wakiongozwa na viongozi wakuu na
maafisa wa Taasisi za TVLA na VVBDRI-TANGA wakiwasili katika shamba la
utafiti Mivumoni lililopo Wilayani Pangani Mkoani Tanga lenye ukubwa wa
ekari 12789.6 ili kuweza kuona shughuli za ufugaji zinazofanyika katika
shamba hilo
Bw.
Warith Al - Kharusi akijadili jambo na wafanyabiashara wenzie wakati
walipokuwa wakitembelea shamba hilo linalofuga Ngo'mbe, mbuzi na Kondoo,
ambapo mpaka sasa Taasisi ya VVBDRI - Tanga imeweza kutumia asilimia 20
ya shamba hilo kwaajili ya shughuli za ufugaji na sehemu inayobaki bado
haitumiki.
Dkt.
Mramba akielezea utengenezaji wa marobota ya nyasi kwaajili ya malisho
ya mifugo na uhifadhi wake unavyofanyika katika shamba hilo, ambapo
Wafanyabiashara hao walivutiwa nazo na kuonesha nia ya kuwekeza katika
katika uzalishaji huo ili shamba hilo ambalo sehemu kubwa ya eneo lake
halijafanyiwa matumizi liweze kuzalisha nyasi hizo kwa wingi kupitia
teknolojia za kisasa na kuweza kuwa na tani za kutosha kusafirisha
kwaajili ya mauzo nje ya nchi
===================================================
Wakati
huo huo wafanyabishara hao pia walitembelea katika kiwanda cha
kuzalisha maziwa "TANGA FRESH LTD" kilichopo eneo la Kange Jijini Tanga
Mkuu
wa Idara ya Fedha katika kiwanda cha Tanga Fresh BW. Clemence Winfredy
akiukaribisha ujumbe wa wafanyabiasha kutoka Oman waliotembelea kiwanda
hicho ili kujionea shughuli za uzalishaji
Bw.Clemence
Winfredy akiwasilisha taarifa ya shughuli za uzalishaji wa kiwanda
pamoja na kuainisha fursa za uwekezaji zinazopatikana katika kiwanda
hicho
Sehemu
ya wafanyabishara wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa ambapo pia
waliweza kushauri baadhi ya maboresho kwaajili ya kuongeza uzalishaji na
usindikaji wa maziwa
Wafanyabiashara wakitembelea eneo la uzalishaji wa maziwa
Wakiangalia na kupokea maelezo namna uzalishaji wa maziwa unavyofanyika hadi hatua ya kufungasha na kwenda sokoni
Matanki kwaajili ya kuhifadhia maziwa yaliyokwisha kamilisha hatua zote za utayarishaji na kuwa tayari kwa kufungashwa
Ujumbe wa wafanyabiashara ukiondoka mkoani Tanga mara baada ya kukamilisha ziara.
No comments:
Post a Comment