leo April 8 2016 Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam kupitia kwa Kamishna Simon Sirro,
limetangaza kuwakamata majambazi 63 wa matukio ya unyang’anyi wa
kutumia silaha katika oparesheni iliyofanyika ndani ya wiki moja.
Kamanda sirro amesema ‘Tarehe
07/04/2016 majira ya saa 09:15 usiku katika eneo la Vingunguti uwanja
wa Koroni, Kikosi maalum cha kupambana na majambazi kilifanikiwa
kukamata silaha aina ya SMG iliyokatwa kitako katika bonde la mto
msimbazi‘
‘katika
tukio lingine, tarehe 4/4/2016 majira ya saa 08:45 asubuhi katika
barabara ya Ally Bin Said, Askari wakiwa kwenye operesheni ya kusaka
wahalifu wa makosa mbalimbali katika wilaya ya Kinondoni, walifanikiwa
kukamata silaha mbili Rifle ambazo hazikuwa na risasi ‘ Simon Sirro
Baada ya
kuyataja matukio yote yaliyopelekea kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa
ujambazi, kamanda Sirro pia hakuacha kuliongea hili la kesho katika
mechi ya Yanga dhidi ya Al-Alhly ya Misri
‘Jeshi
la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi tumejipanga ipasavyo
kuhakikisha mechi hiyo inachezwa katika hali ya usalama, na natoa
tahadhari kuwa hairuhusiwi kwa shabiki yoyote kuingia uwanjani akiwa na
vifaa vya hatari kama Mapanga N.k‘ Simon Sirro
No comments:
Post a Comment