Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amemsweka rumande
Muhandisi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Simoni Ngagani, baada
ya kupuuza agizo lake la kufanya maandalizi mapema ya kununua kokoto na
Saruji kwa ajili ya kusimika mapipa 50 ya kutunzia uchafu kwenye mitaa
mbalimbali katika manispaa ya Shinyanga ikiwemo eneo la kituo cha mabasi
yaendayo wilayani.
Tukio
hilo limetokea jana asubuhi mjini Shinyanga wakati mkuu huyo wa wilaya
akiwa na msafara wake alipowasili katika eneo la stendi ya mabasi
yaendayo wilayani kwa lengo la kufanya uzinduzi wa kusimikwa kwa mapipa
hayo na kukuta maandalizi hayajakamilika.
Matiro
alimuagiza Mhandisi huyo kufanya maandalizi hayo mapema mbele ya
mkurugenzi wake wa manispaa ya Shinyanga Kalinjuna Lewis, kuwa ataandaa
vifaa hivyo majira ya saa moja asubuhi ili zoezi kukusimika mapipa hayo
likamilike haraka, na baada ya hapo wafanye usafi wa mazingira lakini
agizo lake mhandisi huyo akapuuza.
Mkuu
huyo alipomhoji mhandisi huyo kwanini alipuuzia agizo lake la kufanya
maandalizi mapema, mhandisi huyo alianza kujikanyaga kanyaga akidai
sababu iliyomkwamisha ni kukosekana kwa pesa za kununua kokoto na saruji
kwani mvua kubwa ilinyesha na kushindwa kwenda benki, na alivyoamka
asubuhi ndipo atakafuta dhana hizo.
Hata
hivyo mkuu huyo hakuridhika na majibu hayo ndipo DC alipochukua uamuzi
ya kumsweka rumande kwa kumuagiza mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya
Shinyanga kumkamata na kumuweka ndani mhandisi huyo wa ujenzi manispaa
hiyo Samson Ngagani kwa kosa la kuchelewesha maandalizi ya vifaa vya
ujenzi vilivyopangwa kutumika kusimika mapipa ya taka.
“Hawezekani
tukubaliane tuamke mapema ili tufanye kazi hii haraka na pia tuingie
Mitaani kufanya usafi, ambapo mimi nimeamka saa 11 nikajiandaa harafu
wewe una kuja saa mbili tena bila ya kufanya maandalizi yeyote hii si
kunidharau hivyo naagiza OCD mkamate akakae Rumande kwanza ili liwe
fundisho kwa wengine” ,alisema Matiro.
Katika
uzinduzi huo Matiro alisema mapipa hayo ya taka ambayo idadi yake ni
zaidi ya 50 yatawekwa katika maeneo mbali mbali ya manispaa ya Shinyanga
na wananchi wanatakiwa kuyalinda. Awali akiongea katika uzinduzi huo,
mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna alisema mapipa hayo
yamepatikana kutokana na wadau mbali mbali kujitolea kuchangia baada ya
kuhamasishwa na mkuu huyo wa wilaya ambapo pipa moja limegharimu
shilingi elfu 90.
Naye
afisa afya wa manispaa ya shinyanga Elly Nakuzelwa alisema lengo la
kuweka mapipa hayo ya taka ni kuhakikisha manispaa ya Shinyanga inakuwa
katika hali ya usafi ili kuondoa magonjwa ya miripuko yanayosababishwa
na uchafu ikiwemo kipindupindu. Habari na Marco Maduhu na Veronica
Natalis-Malunde1 blog Angalia hapa chini picha yaliyojiri katika
uzinduzi huo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimhoji Mhandisi wa
ujenzi wa manispaa ya Shinyanga Simon Ngagani (katikati mwenye kaunda
suti)kwa kupuunza agizo lake la kufanya maandalizi mapema ya kununua
vifaa vya ujenzi vya kusimikia Mapipa ya uchafu 50 katika mitaa
mbalimbali ya Mji wa Shinyanga ,na mwenye traksuti kushoto ni Mkurugenzi
wa Manispaa hiyo Kalinjuna Lewis akishuhudia Mtumishi wake akikamuliwa
Jipu na hatimaye kuswekwa rumande kwa kumpuuza DC huyo-Picha zote na
Marco Maduhu-Malunde1 blog
Mhandisi wa manispaa ya Shinyanga Simon Ngagani akijitetea kwa mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(kulia),kushoto ni mkurugenzi wa
manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna akisikiliza utetezi wa mhandisi
wake japo aliambulia kuwekwa rumande
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiongea na wananchi kabla
ya kuanza zoezi la kusimika mapipa hayo ya uchafu huku akiwaasa
wayahifadhi na kutoyauza kama vyuma chakafu.
Mwananchi
akila Miguu ya kuku kwenye zoezi la kusimika mapipa hayo huku mkuu wa
wilaya ya Shinyanga akitoa elimu ya kuhifadhi mazingira kwa kutumia
mapipa hayo ya uchafu.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akichanganya zege kwa ajili ya kusimika mapipa ya uchafu Kushoto ni Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna akishiriki zoezi la kusimika mapipa hayo ya uchafu.
Meneja
wa benki ya CRDB tawi la Shinyanga Said Pamui,ambaye ni miongoni mwa
wadau waliochangia mapipa hayo akishiriki zoezi la kusimika
mapipa,aliyeshikilia koleo kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Josephine Matiro.
Meneja
wa benki ya CRDB tawi la Shinyanga Said Pamui,ambaye ni miongoni mwa
wadau waliochangia mapipa hayo akishiriki zoezi la kusimika mapipa
Baada ya kumaliza kuzindua zoezi la kusimika Mapipa ya uchafu, Mkuu
huyo wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alianza kukagua Mazingira
ya eneo la stendi ya Mabasi ya kwenda wilayani na kukuta hali mbaya ya
uchafu ,huku choo cha standi hiyo kikitisha kwa uchafu kama unavyoona
kwenye picha hapo juu na hapa chini,ambapo chemba za vyoo zimeziba kwa
vinyesi, hali ambayo ilimfanya mkuu huyo wa wilaya kumuagiza Mkurugenzi
afanye usafi haraka ndani ya wiki moja akute pasafi
Choo cha stendi ya mabasi yaendayo wilayani kikiwa kimezungukwa na
uchafu yakiwemo maji machafu yaliyotuama,pichani ni afisa mazingira wa
manispaa ya Shinyanga Elly Nakuzelwa akiingia katika choo hicho Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akishuhudia uchafu katika eneo la stendi ya mabasi yaendayo wilayani mjini Shinyanga. Uchafu ukiwa katika choo cha stendi hiyo Chemba ya choo ikiwa imeziba Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog
No comments:
Post a Comment