DKT.KIGWANGALLA AKAGUA HOSPITALI YA TAIFA YA KIFUA KIKUU KIBONG'OTO ILIYOPO KILIMANJARO - LEKULE

Breaking

13 Apr 2016

DKT.KIGWANGALLA AKAGUA HOSPITALI YA TAIFA YA KIFUA KIKUU KIBONG'OTO ILIYOPO KILIMANJARO

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla, ametembelea Hospitali ya Taifa ya Kifua Kikuu Kibong'oto eneo la Sanya Juu Wilani Siha Mkoani Kilimanjaro.

Dkt. Kigwangalla katika Hospitali hiyo, alipata kitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo wodi za wagonjwa wa Kifua Kikuu (TB) ya kawaida na ile kali ambapo pia aliweza kutembelea eneo la kituo cha utafiti cha magonjwa hayo pamoja na Maabara.

Kihistoria Hospitali hiyo ya Kibong’oto ilifunguliwa rasmi 29 Oktoba mwaka 1952 na Lady Twining, baada ya miaka saba ya vita ya pili ya dunia chiniya utawala wa Muingereza na imekuwa ikitoa huduma hiyo ya magonjwa ya kuambukiza hususani Kifua Kikuu.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga amemwelezea Naibu Waziri changamoto mbalimbali ikiwemo suala la nyumba za watumishi na mambo mengine ikiwemo suala la bajeti ya vifaa tiba.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitia saini kitabu cha wageni katika Hospitali ya Taifa ya Kifua Kikuu Kibong'oto ilipo Mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yake 10 Aprili 2016. Anayeshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipata maelezo ya kitaalam kutoka kwa msimamizi wa Maabara ya Hospitali hiyo ya Kibong'oto.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipatiwa maelezo ya kina namna ya vifaa hivyo vinavyofanya kazi katika upimaji wa kifua kikuu kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga.
Eneo la Utafiti wa magonjwa ya kuambukiza katika Hospitali hiyo ya KIbong'oto.....Wakitoka katika jengo la Utafiti.
Msafara ukielekea upande wa wadi za wagonjwa wa TB sugu.
Moja ya alama zinazoelekeza maeneo ya Hospitali hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Kibong'oto, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga akimuongoza Naibu Waziri wa Afya na watendaji mbalimbali kuelekea katika eneo wanalohudumia wagonjwa wenye Kifua kikuu (TB) sugu.
Wafanyakazi wa Hospitali hiyo ya Kibong'oto na wageni wengine wakielekea katika eneo la TB sugu wakati wa ziara hiyo ya Naibu Waziri wa Afya.Mkuu wa wilaya ya Siha,Dkt Charles Mlingwa (katikati) wakielekea katika eneo hilo la TB sugu wakati wa ziara hiyo ya Naibu Waziri wa Afya.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipatiwa maelezo ya kina juu ya wagonjwa wa TB sugu waliopo ndani ya wodi (hawapo pichani) kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga.
 Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga akionyeshaa namna wodi hizo zinavyofanya kazi na jinsi wanavyotoa huduma.
 
Msafara huo ukirejea katika maeneo mengine wakati wa ukaguzi na Naibu Waziri wa Afya Dk.Kigwangalla.

Pichani wote waliovaa 'mask' maalum ni kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya vijidudu vya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) hasa kwa upande huo wa wagonjwa maalum wa TB sugu.ambao wapo upande maalum. Hivyo kuvaa kifaa hicho kinasaidia kupunguza hali ya maambukizo wakati wa kufika eneo hilo kama sheria na taratibu zilizowekwa kitaalam na uongozi wa Hospitali hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipata maelezo mafupi kutoka kwa wataalam wa Hospitali hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipata maelezo mafupi kutoka kwa wataalam wa Hospitali hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitoa maagizo kwa uongozi wa Hospitali hiyo.


Mtaalam wa magonjwa ya kuambukiza, wa Hospitali ya Kibong'oto ,Dkt. Stella Mpagama akimkabidhi kitabu chake Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Hamisi Kigwangalla. (Picha zote na Andrew Chale).

No comments: