Idara ya Afya nchini Marekani imetoa ushauri mpya kuhusiana na uja uzito na virusi vya Zika.
Idara
hiyo kwa sasa inapendekeza kuwa wanawake wanaogunduliwa kuwa na virusi
vya Zika wasubiri hadi majuma nane baada ya dalili kuonekana kabla
hawajaanza juhudi za kushika mimba tena.Ushauri kwa wanaume nao kuwa wanapaswa kusubiri hadi miezi sita kabla yakujaribu kuzalisha.
Virusi hivyo husambazwa kwa njia ya mbu kwa kawaida ingawa wanasayansi sasa wamesema kuwa vinaweza kusambazwa kupitia tendo la ngono.
Maradhi hayo yamesambaa katika maeneo ya kusini mwa Marekani na visiwa vya Caribbean ambapo watoto wanaozaliwa na ulemavu, hasa kichwa kuwa kidogo kuliko kawaida.
No comments:
Post a Comment