Mahakama
ya hakimu mkazi Singida imewahukumu washitakiwa sita adhabu ya kutumikia
jela jumla ya miaka 120 na kulipa faini ya jumla ya zaidi ya shilingi
Bilioni 1.4, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumiliki kinyume na
sheria vipande 53 vya tembo vyenye thamani ya shilingi 149,336,000 na
kosa la jingine la uwindaji.
Washitakiwa
hao ni Eliud Selema Mayunga (38) mkazi na mkulima wa kijiji cha
Kiombo,Ramadhani Said Biladuka (47) mkulima mkazi wa Itigi,Lenard Oscar
Sunzu (31) mkazi wa kijiji cha Karangari,Pilimon Michael Kanyonga (31)
mkazi wa Kitaraka Itigi,Iddi Waziri Issah Ustadh (30) mkazi wa kijiji
cha Kiombo na Jimmy Charles Lyimo (39) mfanyabiashara wa Tabora Kyombo.
Mwendesha
mashitaka na mwanasheria wa serikali Petrida Mutta alidai mbele ya
hakimu mfawidhi mwandamizi wa mahakama hiyo, Jocye Minde kuwa mnamo
Machi, 31 mwaka 2014, muda usiojulikana washitakiwa kwa pamoja
walikamatwa wakiwa wamehifadhi na kumiki vipande hivyo 53 vya meno ya
tembo nyumbani kwa mshitakiwa Issa Ustadh, huku wakijua wazi kuwa
kitendo hicho ni kinyume na sheria.
Kabla ya
kutolewa kwa adhabu hiyo mwanasheria wa serikali, Mutta aliiomba
mahakama hiyo kuwapa washitakiwa adhabu kali ili iwe fundisho kwao.
“Mheshimiwa
kwa sasa tunaendelea kusikia na kuona vitendo vya uwindaji na biashara
za nyara za serikali vikiendelea kushamiri, vitendo hivi haviwezi
kufumbiwa macho kwa sababu vikifumbiwa macho, fahari ya nchi hii ya
wanyama pori itatoweka naiomba mahakama yako itoe adhabu kali si tu iwe
fundisho kwa washitakiwa mbali iweze kuwaonya na watu wengine wanaotaka
kujihusisha na uwindaji na biashara haramu ya nyara za serikali,”
alisema mwanasheria huyo wa serikali.
Kwa
upande wa washitakiwa ambao wakili wao Mr. Josephat Raphael Wawa
hakuwepo wakati hukumu hiyo inatolewa kila mmoja kwa nafasi yake
aliiomba mahakama hiyo impe adhabu nafuu.
Akitoa
hukumu hiyo iliyosikilizwa na umati mkubwa wa wananchi, hakimu Minde
alisema upande wa jamhuri imethibitisha bila kuacha shaka yoyote kwamba
washitakiwa wanayo hatia kwa makosa yote mawili.
“Kwa kosa
la kwanza la kumiliki kinyume na sheria vipande 53 vya meno ya
tembo,kila mmoja wenu atatumikia jela miaka 20 na kila mmoja wenu,
atalipa faini ya shilingi 248,893,333.30 kwa kosa la pili la kujihusisha
na uwindaji haramu,kila mmoja wenu,” alisema hakimu
No comments:
Post a Comment