March 31 2016 Taasisi ya kupambana na Rushwa TAKUKURU iliwafikisha Mahakamani Kisutu Dar es salaam Wabunge wa CCM Victor Mwambalaswa wa Lupa, Kangi Lugola wa Mwibara na Sadiq Murad wa Mvomero kwa kosa la kuomba rushwa ya milioni 30.
Waliomba
hiyo rushwa kutoka kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya
Gairo kama kishawishi cha kutoa mapendekezo mazuri kwenye ukaguzi wa
hesabu zake za mwaka 2015/16 ambapo Mahamani March 31 Wabunge hao walipata dhamana ya shilingi milioni tano na kesi hiyo itatajwa tena April 14 2016.
No comments:
Post a Comment