Ikiwa zimepita wiki mbili tangu kutokea
kwa ajali Kimara Dar es salaam, Usiku wa kuamkia March 25 kumetokea
ajali nyingine Kimara Baruti ambapo basi la Princes Muro lenye usajili namba T 551 BQP limevamia kituo kipya cha abiria.
Taarifa rasmi zinasema kuwa basi hilo
lilokuwa likitokea Arusha kuja Dar es salaam halikuwa na abiria wala
hakuna aliyefariki, kwa mujibu wa muhusika wa basi hilo alisema wakati
basi hilo lilipopata itilafu maeneo ya mto Wami wahusika walichukua
uamuzi wa kuwaamisha abiria wote kutoka kwenye basi hilo na kuwapeleka
kwenye basi lingine kwahiyo mpaka linaingia Dar na kupata ajali halikuwa
na abiria.
No comments:
Post a Comment