Michezo Misri wametoka salama Nigeria, kazi imebakia kwa Taifa Stars Septemba 2 2016 - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Saturday, 26 March 2016

Michezo Misri wametoka salama Nigeria, kazi imebakia kwa Taifa Stars Septemba 2 2016Bado kivumbi cha mataifa ya Afrika kuendelea kuwania nafasi ya kuelekea fainali za AFCON 2017 Gabon kinaendelea, March 25 2016 hatua ya Makundi ya kuwania kufuzu michuano hiyo iliendelea kama kawaida.
Kwa upande wa watanzania walikuwa wanaangalia mchezo wa Kundi G kati ya Nigeria dhidi ya Misri, kwani hili ndio kundi waliomo pamoja na Chad, hivyo dua zao zilikuwa nikuomba mchezo huo umalizike kwa sare ya aina yoyote ile, ili kutoweka tofauti ya point nyingi dhidi ya timu hizo.
Nigeria ambao walikuwa na nafasi ya pili wakiwa na point nne sawa na Tanzania wameshindwa kuibuka na ushindi dhidi ya Misri licha ya kuwa walikuwa nyumbani, ila wameishia kuambulia sare ya goli 1-1, Nigeria walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 60 kupitia kwa Oghenekaro Etebo, ila Misri walisawazisha dakika ya 90 kupitia Mohamed Salah.
kundi
Huu ndio msimamo wa Kund G ulivyo kwa sasa
Kwa sasa Misri wanaendelea kuwa kileleni mwa Kundi G wakifuatiwa na Nigeria, lakini mtihani unabakia kwa timu ya taifa ya Tanzania ambayo inahitaji nafasi ya kushiriki AFCON 2017 Gabon, ila mchezo wake wa marudiano dhidi ya Nigeria Septemba 2 unatabiriwa kuwa utakuwa mgumu.
Post a Comment