Ligi ya Wanawake yaja - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Sunday, 13 March 2016

Ligi ya Wanawake yaja

 Shirikisho la Soka nchini (TFF) lipo katika mchakato wa kuanzisha Ligi Kuu ya Wanawake itakayoanza muda wowote mwaka huu.

Hayo yalisemwa jana na Rais wa TFF, Jamal Malinzi wakati wa mkutano mkuu wa shirikisho hilo uliofanyika kwenye Hoteli ya Naivera jijini Tanga.

Malinzi alisema kuwa mbali na ligi hiyo, pia mwaka huu itaanzishwa Ligi Kuu ya vijana chini ya miaka 20 na kufuta mashindano ya Kombe la Uhai na tayari mchakato wa kupata wadhamini kwa ajili ya ligi hizo mbili umeanza.

“Mara kadhaa tumekuwa tukipigiwa kelele juu ya ligi ya wanawake, ambayo hatujawahi kuwa nayo, ila msimu huu kwa maana ya msimu ujao ligi hiyo itakuwa imeanza pamoja na ligi ya vijana hivyo hatutakuwa na michuano ya Kombe la Uhai,” alisema Malinzi Malinzi.
Post a Comment