NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
POLISI
wamelazimika kufyatua mabomu ya machozi ili kuwatawanya watu
waliojikusanya mbele ya Benki ya CRDB tawi la Mbagala - Rangi Tatu,
baada ya mtu mmoja aliyekuwa akiongea na simu ndani ya benki hiyo
kukaidi maagizo ya polisi ya kuacha kufanya hivyo mapema leo mchana wa
Machi 11, 2016.
Kwa
mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, watu watatu mmoja akiongea na
simu na wengine wawili waki-chat ndani ya benki hiyo, waliagizwa na
mlinzi wa benki kuacha kufanya hivyo lakini wakakaidi.
Baada
ya mlinzi kuona hivyo alitoa taarifa kituo cha polisi Mbagala -
Maturubai, na hapo polisi wakiwa ndani ya gari lao maarufu kama
defender, waliwasili kwenye eneo hilo na kuamuru watu hao ambao
wanaelezwa kuwa wateja, kutoka ndani ya benki hiyo.
Hata hivyo palitokea mabishano baada ya mmoja wao kukaidi amri ya polisi na kuanza kupigana nao.
Kuona
hivyo watu walianza kujaa na polisi bila kufanya ajizi wakafyatua
mabomu ya machozi kutawanya watu na kuwadhibiti 'wateja' hao wabishi na
hatimaye kufanikiwa kuondoka nao.
Hali
hiyo ilizua tafrani huku watu wakidhani kuwa palikuwepo na tukio la
ujambazi, kwani ni mwezi uliopita umbali wa mita chache kutoka kwenye
benki hiyo, palitokea tukio baya ya uvamizi wa benki ya Access ambapo
watu saba waliauawa, wakiwemo polisi.
No comments:
Post a Comment