INAFRIKA BAND AKA “WAZEE WA INDEGE” KUTUMBUIZA MAREKANI (FESTIVAL OF NATIONS) - LEKULE

Breaking

13 Mar 2016

INAFRIKA BAND AKA “WAZEE WA INDEGE” KUTUMBUIZA MAREKANI (FESTIVAL OF NATIONS)

7e6c7f86-d634-4da9-af7d-b83958f68951
Bendi maarufu Inafrika band aka Wazee wa Indege wanatarajiwa kuruka wakati wowote ule kuelekea nchini marekani kushiriki katika maoyesho makubwa ya kimataifa ya Festival of nations ,yatakayo fanyika katika Dollywood Theme Park,bendi hii kutoka Tanzania ndio bendi pekee iliyoteuliwa kuliwakilisha bara la Afrika katika maonyesho hayo ya kimataifa.
Inafrika band itakuwepo nchini marekani katika ziara ya kikazi kwa muda wa miezi mitatu kuzikonga nyoyo za washabiki wa kimataifa nchini marekani.
Kuchaguliwa kwa Inafrika band kushiriki maonyesho hayo makubwa kunatokana na mvuto wa muziki wa bendi hiyo kukubalika zaidi kimataifa.
Muziki ambao una maadili ya kitanzania ambako nje ya mipaka umewateka
washabiki wengi wa kimataifa.  
Bendi hiyo yenye makao jiji Dar-es-salaam imejikuta haina muda wa kupumzika kutoka na wingi Tour za kimataifa kwa muda wa miaka 10 sasa.
Ni kama wiki mbili tu bendi hiyo imerudi kutoka safari ya nchi 19 za bara la ulaya. Tunawatakia kila la heri Inafrika Band aka Wazee wa Indege katika kutuwakilisha huko Marekani. Bendi hiyo ilikuwapo Dollywood ,Marekani mwaka 2014 na kuwanasa washabiki wengi  na muziki wao wa kitanzania\

No comments: