EU yafuta misaada kwa Burundi - LEKULE

Breaking

14 Mar 2016

EU yafuta misaada kwa Burundi

Muungano wa ulaya umefutilia mbali ufadhili wowote wa moja kwa moja kwa serikali ya Burundi.
Uamuzi huu unafuatia wasiwasi kuhusu rekodi ya haki za binadamu ya watawala wa sasa wa nchi hiyo.
Takriban watu 400 wameuwaa tangu rais Pierre Nkurunziza atangaze kuwania muhula wa tatu kama rais mwezi Aprili mwaka uliopita.


Wapinzani wake walimkashifu wakisema kuwa kauli hiyo inakiuka katiba ya nchi .
Ghasia ziliibuka upande wa upinzani ulipoandaa maandamano kupinga hatua ya Nkurunziza ambaye alijibu kwa kutuma vikosi vya kupambana na ghasia kuvunja maandamano.
Hali iligeuka na kuwa mbaya pale kulikotokea jaribio la mapinduzi yaliyozimwa kwa jeshi makabiliano yaliyopelekea mamia ya watu kuuawa.




Mungano wa ulaya ulisema kuwa ulitaka serikali ya Burundi kuchukua hatua madhubuti kumaliza ghasia nchini humo.
Unasema kuwa utaendela kutoa misaada kwa watu wa Burundi bila ya kutumia mifumo ya serikali tawala.

No comments: