Azam imejipatia ushindi wa mabao 3-0 ndani ya dakika 9 dhidi ya wapinzani wao klabu ya Bidvest.
Mchezo
huo ulianza kwa kasi kwa timu zote kushambuliana huku Azam wakionekana
kujiamini zaidi licha ya kuwa ugenini na kusukuma mashambulizi ya nguvu,
ambapo hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, timu zote zilikuwa
hazijafungana.
Nahodha wa Azam,John Boko
Mabao
ya Azam yaliyopatikana kipindi cha pili yamefungwa na Salum Abubakary
Sure Boy katika dakika ya 51 kwa shuti kali nje ya eneo la 18 kufuatia
kona iliyochongwa na Messi na kuokolewa vibaya na mabeki wa Wits.
Shomari
Kapombe akafunga bao la pili dakika ya 56 baada ya mabeki wa Wits
kufanya uzembe na mfungaji huyo akaserereka chini na kupiga shuti
lililomshinda kipa wa Wits na dakika 3 baadaye nahodha John Bocco
akifunga bao la tatu dakika ya 59.
Azam
FC iliweza kucheza kandanda safi kwa takribani muda wote huku
ikishangiliwa na watanzania takribani 200 wanaoishi nchini Afrika
Kusini.
Kwa
matokeo hayo, njia sasa ni nyeupe kwa Azam kusonga mbele, kwani
itahitaji sare aina yoyote au isifungwe zaidi ya 3-0, katika mchezo wa
marudiano utakaopigwa Chamazi jijini dare s salaam, ili isonge mbele.
No comments:
Post a Comment