Wanahabari na Watafiti kutoka Tume ya
Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), waliokuwa katika ziara ya
kuzungumza na wakulima wa mkoa wa Mwanza kuhusu changamoto za kulimo
zinazo wakabili pamoja na matumizi ya bioteknolojia katika kilimo wakiwa
mbele ya kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
walipozuru kaburi hilo hivi karibuni Kijiji cha Mwitongo Butiama mkoani
Mara.
Watafiti na wanahabari hao wakiwa mbele ya makaburi ya wazazi wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
Mtafiti Kiongozi wa Tume ya Taifa ya
Sayansi na Teknnolojia (Costech), Dk.Nicholaus Nyange (kushoto), na
Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Emmarold
Mneney wakiwa wamesimama ilipo sanamu ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Nyerere.
Hapa ni picha ya pamoja katika sanamu ya Baba wa Taifa.
Matembezi yakiendelea katika makazi ya Baba wa Taifa.
Mratibu Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Afrika, Daniel Otunge (kushoto) Mtafiti
Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknnolojia (Costech),
Dk.Nicholaus Nyange (katikati), na Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la
Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Emmarold Mneney wakiwa wamekaa katika kibanda alichokuwa akipenda kupumzika Hayati Nyerere wakati wa
uhai wake.
Jamii inayofanya shughuli mbalimbali
nyumbani kwa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere wakionesha
upendo kwa kunywa chai pamoja katika makazi ya Mwalimu Nyerere yaliyopo
Kijiji cha Mwitongo, wilayani Butiama mkoani Mara kama walivyonaswa na
kamera yetu katika ziara hiyo.
Picha ya pamoja katika nyumba maalumu lilipo kaburi na Mwalimu Nyerere.
Dereva wa Msafara huo, Mr Stanley akiwa
mbele ya gari na mtafiti Kutoka Kituo cha Utafiti cha Ukiriguru cha
jijini Mwanza, Isabela Msuya.
No comments:
Post a Comment