Mamia ya barua na picha zinazosimulia kuhusu uhusiano wa karibu kati ya Papa John Paul II na mwanamke aliyeolewa zimeoneshwa kwa BBC.
Urafiki huo ulidumu kwa miaka 30.
Barua hizo alizomwandikia mwanafalsafa Mmarekani, ambaye ni mzaliwa wa Poland, Bi Anna-Teresa Tymieniecka zimewekwa faraghani katika Maktaba ya Taifa ya Poland kwa miaka mingi.
Zinafichua sura nyingine ya maisha ya kiongozi huyo wa kidini, aliyefariki mwaka 2005.
Hata hivyo, hakuna ishara zozote kwamba Papa alikiuka kiapo chake cha useja.
Urafiki wao ulianza 1973 pale Bi Tymieniecka alipowasiliana na Papa huyo, wakati huo akiwa Kadinali Karol Wojtyla, aliyekuwa akisimamia Jimbo Kuu la Krakow, kuhusu kitabu cha filosofia ambacho kiongozi huyo wa kidini alikuwa amekiandika.
Mwanamke huyo aliyekuwa wakati huo na umri wa miaka 50 alisafiri kutok Marekani hadi Poland kujadili kitabu hicho.
Baadaye, wawili hao walianza kuwasiliana. Mwanzoni, barua za kadinali huyo zilikuwa rasmi, lakini uhusiano wao ulipoendelea kuimarika, zikawa za undani zaidi.
Wawili hao walianza kushirikiana katika kuandika upya kitabu cha kadinali huyo na walikutana mara nyingi, wakati mwingine karani wa kadinali huyo akiwa, na wakati mwingine peke yaao.
Pia waliwasiliana mara kwa mara.
Mwaka 1974, aliandika kwamba alikuwa akisoma tena na tena barua nne kati ya alizoandikiwa na Bi Tymieniecka katika mwezi mmoja kwa sababu „zilikuwa na maana sana na zilikuwa za undani”.
Picha ambazo hazijawahi kuonyesha hadharani kwa umma zinamuonyesha Karol Wojtyla akiwa ametulia sana.
Alimwalika Bi Tymieniecka ajiunge naye katika matembezi na katika likizo akiteleza kwenye theluji. Wakati mmoja, alijiunga naye katika safari ya kwenda na kupiga hema. Picha zinaonyesha mwanamke huyo akimtembelea Vatican.
Katika barua moja Septemba 1976, Kadinali Wojtyla anaandika: "Mpendwa Teresa, nimepokea barua zote tatu. Unaandika kuhusu kutamauka, lakini sikupata jibu kuhusu maneno hayo.”
Anamweleza kama “zawadi kutoka kwa Mungu”.
BBC haijaona barua zozote za Bi Tymieniecka. Lakini inaaminika ziliuziwa Maktaba ya Taifa ya Poland na Bi Tymieniecka mwaka 2008, miaka sita kabla yake kufariki.
Lakini hazikuwa pamoja na barua zilizoandikwa na Papa ambazo BBC ilioneshwa.
Kadinali Wojtyla alikuwa na marafiki kadha wengine wa kike, akiwemo Wanda Poltawska, mtaalamu wa masuala ya akili ambaye waliwasiliana naye kwa miongo kadha.
Lakini kwenye barua zake kwa Bi Tymieniecka anaonekana wakati mwingine kuguswa sana n ahata kutatizwa na maana ya uhusiano wao.
Papa John Paul II alifariki 2005, baada ya kuongoza Kanisa Katoliki kwa miaka 27. Mwaka 2014 alitawazwa kuwa mtakatifu.
No comments:
Post a Comment