Serikali imekiri kuwepo kasoro nyingi zilizojitokeza katika mradi Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na TASAF ikiwamo ubadhirifu wa fedha kwa Kaya sizizokuwa na sifa kupewa pesa kupitia mpango huo hivyo imejipanga kuborsha zaidi mpango huo katika awamu ya tatu kwa kutengeneza miundombinu mizuri ya kutambua Kaya zinazolengwa.
Akijibu swali la Mhe.Magdalena Hamisi Sakaya Mbunge wa Kaliua (CUF) lililouliza ni vigezo gani vinatumika kuondoa Kaya zilizopendekezwa kwenye mradi na kubakiza Kaya chache, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki amesema mpango wa kunusuru Kaya maskini hutambulishwa kijijini na wataalam kutoka Halmashauri husika kwa kusimamiwa na uongozi wa kijiji kisha kuweka vigezo vya Kaya maskini.
“ Wakusanya taarifa huchaguliwa kutoka miongoni mwa vijana wanaoishi kijijini hapo na kupitia nyumba kwa nyumba kuorodhesha Kaya ambazo zinakidhi vigezo vilivyoanishwa na mkutano wa Kijiji ila bado kuna malalamiko yanayotolewa kuwa Kaya maskini zinaachwa na kupewa Kaya nyingine ambazo sio maskini
"Kwa kuliona tatizo suala hili tunalifanyia uchunguzi na tunaomba watu watoe taarifa ikiwa wataona ukiukwaji wa uorodheshaji wa Kaya zitakazohusika na mpango huu ili hatua ziweze kuchukuliwa dhidi ya yoyote atakaye bainika kufanya hivyo
“Mpaka sasa kutokana na malalamiko yaliyojitokeza katika kuorodhesha Kaya maskini zinazotakiwa kuwezeshwa na mpango huu tumewawajibisha watendaji toka Wilaya za Karagwe, Kagera , kibondo na Kigoma na tuomba kupewa taarifa kwa sehemu yoyote ambapo kutatokea tatizo kama hili na tutachukua hatua mara moja kuokoa fedha zilizotakiwa kwenda kusaidia watu husika” Alisema Mhe Angella Kairuki.
Aidha Mhe. Angella Kairuki ameongeza kuwa kuna taarifa zinazoenezwa kuwa fedha za mpango wa TASAF Awamu ya Tatu ni fedha za freemasons, taarifa hizo sio za kweli kwani fedha hizi zinatolewa na Serikali ili kusaidia Kaya maskini ili ziweze kujikwamua kiuchumi kwa kuweza kupata Elimu Malazi na chakula bora.
TASAF ni mpango wa kunusuru Kaya maskini na imekuwa katika awamu tatu mpaka hadi sasa kwa ajili ya kuwezesha Kaya maskini kujikwamua kiuchumi.
No comments:
Post a Comment