Hello

Welcome lekule blog

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation.
together in the world. #lekule86
Join us on

Rais Magufuli Asema Yeye si Kichaa wala Dikteta......Aahidi Kuifanyia Mema Nchi hata Akifa awe Rais wa Malaika


RAIS Dk. John Magufuli amesema anapochukua hatua yeye si kichaa, si dikteta, si shetani wala si mnyama, ila ni mpole, lakini amefika mahali lazima afanye hivyo kwani ndani ya Serikali yanafanyika mambo ya ajabu.

Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam katika kilele cha Siku ya Sheria nchini, alipokuwa mgeni rasmi kwa mara ya kwanza katika uzinduzi wa Mwaka wa Mahakama tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisifu kazi kubwa inayofanywa na Idara ya Mahakama, huku akitangaza uamuzi wa gharama za kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Bunge zaidi ya Sh bilioni nne ni bora zikawasaidia wananchi.

“Ninapochukua hatua mimi si mnyama, si dikteta, si shetani, ni mpole kweli, lakini inafika mahali lazima nifanye, yanayofanyika serikalini ni mambo ya ajabu sana, nataka kutoa sadaka yangu, inawezekana hata nikifa naweza kuwa rais wa malaika,” alisema.

Alipongeza kazi kubwa inayofanywa na mahakama huku akibaki kujiuliza kwanini katika maadhimisho ya siku yao hawarushi matangazo yao moja kwa moja kupitia luninga.

“Mnafanya kazi kubwa, nilipofika niliuliza kwanini hii siku yenu hamrushi ‘live’, nikajibiwa fedha za kurusha ‘live’ zinapelekwa kuwahudumia wananchi.

“Kipindi kimoja kurusha ‘live’ kwa wiki mbili inatumika zaidi ya Sh bilioni nne, ni vizuri kuzikata hizo fedha zinazopelekwa kurusha ‘live’ zikapelekwa katika kesi za ubunge zinazohitaji shilingi bilioni tatu kusikilizwa hadi kumalizika kwake,” alisema.

Alisema mahakama ilikuwa inapewa bajeti ya Sh bilioni 41, lakini mwaka 2015/2016 ilishuka wakatakiwa kupewa Sh bilioni 12 ambazo hadi sasa hawajapewa.

“Kiongozi lazima ufikirie wapi pa kupeleka fedha na wapi pa kunyima, watu wa mahakama mnafanya kazi ya Mungu, nawaahidi ndani ya siku tano nitakuwa nimewapa Sh bilioni 12 zote.

“Sina tatizo la masilahi ya wafanyakazi wa mahakama, katika bajeti ya mwaka huu nitawapa fedha nyingi kuliko bajeti zote zilizopita, fedha zipo,” alisema.

Mahakimu Kutumbuliwa
Rais Magufuli alisema anamwagiza Jaji Mkuu kuwachukulia hatua mahakimu 502 ambao hawakufikia malengo ya kumaliza kesi 250-260 kwa mwaka. Walimaliza kesi chini ya 100.

“Mahakimu ambao hawajafikia kumaliza kesi 260 hayo ndiyo majipu yako Jaji Mkuu, unatakiwa kuyatumbua, wewe uliniapisha hata mimi, leo unapitisha agizo mwingine anapinga.

“Unatoa siku saba sasa sijui ndiyo watamaliza kutoa hizo hukumu, nakuagiza wachukulie hatua, tusipochukua hatua hakuna kitakachofanyika.

“Walioshindwa kufikia lengo unawabakiza wa nini, wasomi wako wengi, hata ukitangaza leo watajitokeza, niruhusu mimi nitangaze, sitaki kuingilia mahakama,” alisema.

Mabilioni ya NIDA
Akizungumzia hatua yake kwa watendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), alisema ilipewa Sh bilioni 176.6, lakini vitambulisho vilivyotengenezwa havifiki hata milioni mbili na havina sahihi wakati vitambulisho vya kupigia kura fedha iliyotolewa haizidi Sh bilioni 70, lakini vina sahihi za wapigakura wote wa Tanzania ambao ni milioni 23,253,982.

“Utaona ugumu wa kuongoza, nchi inatawaliwa na madudu ya kila aina, wapo watu wanacheza na fedha wanavyotaka wakati wapo watu masikini sana, wengine wanataka bodi zao wakakae Ulaya.

“Hapo ndipo tulipofikia, wengine wanalipwa mshahara kwa mwezi Sh milioni 35, naomba mniombee kabla ya kunihukumu, toeni hukumu kwa haki kwa hawa wanaotaka kuifikisha nchi pabaya, toeni hukumu zao haraka,” alisema.

Kesi za Wakwepa kodi
Rais Magufuli alisema kuna kesi 442 za kukwepa kodi ambazo zingeamuliwa Serikali ingepata Sh trilioni moja, ambayo ingeweza kununua ndege zaidi ya sita.

Alimuomba Jaji Mkuu kuzimaliza kesi 442 na kama zikimalizika fedha hizo Sh trilioni moja ataipa Idara ya Mahakama Sh bilioni 259 na Sh bilioni 750 zilizobakia zitanunuliwa ndege sita na wafanyafakazi 250 ATCL waliopo sasa wataondolewa.

Akizungumzia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alisema kuna kesi 26 za watu waliokutwa na nyara za Serikali, ambazo zipo zaidi ya miaka mitano hazijaamuliwa kwa sababu upelelezi bado.

“Polisi wapo, DPP yupo, upelelezi unaendelea kila siku, hapo unaona tatizo lilipo, DPP upo unapeleleza nini au unatafuta rushwa?” alisema.

Alisema suala la kuanzishwa kwa mahakama ya mafisadi ya wahujumu uchumi halihitaji kwenda bungeni kufanya mabadiliko, lifanywe haraka, mahakama ianze kwani nchi inachezewa.

Pamoja na hali hiyo Rais Magufuli alikubali kupokea maombi yote yaliyotolewa na mahakama na kuyazingatia kwani lazima ayaunge mkono ikiwamo kukubali watumishi wa Idara ya Mahakama wasome na kupatiwa mikopo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

“Nimeamua nchi iende na itaenda, anayefikiria ataikwamisha atakwama yeye, nategemea zaidi mahakama katika kufanikisha hilo,” alisema.


Share this:

ABOUTME

Hi all. This is deepak from Bthemez. We're providing content for Bold site and we’ve been in internet, social media and affiliate for too long time and its my profession. We are web designer & developer living India! What can I say, we are the best..

Post a Comment
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.

Labels

LEKULE TV EDITORIALS ARTICLES DC ROBOTICS DIGITAL SEMICONDUCTORS GENERATOR AC EXPERIMENTS MANUFACTURING-ENGINEERING REFERENCE FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY ELECTRONICS ELECTRICAL ENGINEER MEASUREMENT TRANSDUCER & SENSOR VIDEO ARDUINO RENEWABLE ENERGY AUTOMOBILE TEARDOWN SYNCHRONOUS GENERATOR DIGITAL ELECTRONICS ELECTRICAL DISTRIBUTION CABLES AUTOMOTIVE MICROCONTROLLER SOLAR PROTECTION DIODE AND CIRCUITS BASIC ELECTRICAL ELECTRONICS MOTOR SWITCHES CIRCUIT BREAKERS CIRCUITS THEORY PANEL BUILDING ELECTRONICS DEVICES MIRACLES SWITCHGEAR ANALOG MOBILE DEVICES WEARABLES CAMERA TECHNOLOGY COMMUNICATION GENERATION BATTERIES FREE CIRCUITS INDUSTRIAL AUTOMATION SPECIAL MACHINES ELECTRICAL SAFETY ENERGY EFFIDIENCY-BUILDING DRONE CONTROL SYSTEM NUCLEAR ENERGY SMATRPHONE FILTER`S POWER BIOGAS BELT CONVEYOR MATERIAL HANDLING RELAY ELECTRICAL INSTRUMENTS ENERGY SOURCE PLC`S TRANSFORMER AC CIRCUITS CIRCUIT SCHEMATIC SYMBOLS DDISCRETE SEMICONDUCTOR CIRCUITS WIND POWER C.B DEVICES DC CIRCUITS DIODES AND RECTIFIERS FUSE SPECIAL TRANSFORMER THERMAL POWER PLANT CELL CHEMISTRY EARTHING SYSTEM ELECTRIC LAMP FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 2 BIPOLAR JUNCTION TRANSISTOR 555 TIMER CIRCUITS AUTOCAD BLUETOOTH C PROGRAMMING HOME AUTOMATION HYDRO POWER LOGIC GATES OPERATIONAL AMPLIFIER`S SOLID-STATE DEVICE THEORRY COMPUTER DEFECE & MILITARY FLUORESCENT LAMP INDUSTRIAL ROBOTICS ANDROID ELECTRICAL DRIVES GROUNDING SYSTEM CALCULUS REFERENCE DC METERING CIRCUITS DC NETWORK ANALYSIS ELECTRICAL SAFETY TIPS ELECTRICIAN SCHOOL ELECTRON TUBES FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 1 INDUCTION MACHINES INSULATIONS USB ALGEBRA REFERENCE HMI[Human Interface Machines] INDUCTION MOTOR KARNAUGH MAPPING USEUL EQUIATIONS AND CONVERSION FACTOR ANALOG INTEGRATED CIRCUITS BASIC CONCEPTS AND TEST EQUIPMENTS DIGITAL COMMUNICATION DIGITAL-ANALOG CONVERSION ELECTRICAL SOFTWARE GAS TURBINE ILLUMINATION OHM`S LAW POWER ELECTRONICS THYRISTOR BOOLEAN ALGEBRA DIGITAL INTEGRATED CIRCUITS FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 3 PHYSICS OF CONDUCTORS AND INSULATORS SPECIAL MOTOR STEAM POWER PLANTS TESTING TRANSMISION LINE C-BISCUIT CAPACITORS COMBINATION LOGIC FUNCTION COMPLEX NUMBERS CONTROL MOTION ELECTRICAL LAWS INVERTER LADDER DIAGRAM MULTIVIBRATORS RC AND L/R TIME CONSTANTS SCADA SERIES AND PARALLEL CIRCUITS USING THE SPICE CIRCUIT SIMULATION PROGRAM AMPLIFIERS AND ACTIVE DEVICES APPS & SOFTWARE BASIC CONCEPTS OF ELECTRICITY CONDUCTOR AND INSULATORS TABLES CONDUITS FITTING AND SUPPORTS ELECTRICAL INSTRUMENTATION SIGNALS ELECTRICAL TOOLS INDUCTORS LiDAR MAGNETISM AND ELECTROMAGNETISM PLYPHASE AC CIRCUITS RECLOSER SAFE LIVING WITH GAS AND LPG SAFETY CLOTHING STEPPER MOTOR SYNCHRONOUS MOTOR AC METRING CIRCUITS BECOME AN ELECTRICIAN BINARY ARITHMETIC BUSHING DIGITAL STORAGE MEMROY ELECTRICIAN JOBS HEAT ENGINES HOME THEATER INPECTIONS LIGHT SABER MOSFET NUMERATION SYSTEM POWER FACTORS REACTANCE AND IMPEDANCE INDUCTIVE RECTIFIER AND CONVERTERS RESONANCE SCIENTIFIC NOTATION AND METRIC PREFIXES SULFURIC ACID TROUBLESHOOTING TROUBLESHOOTING-THEORY & PRACTICE 12C BUS APPLE BATTERIES AND POWER SYSTEMS DC MOTOR DRIVES ELECTROMECHANICAL RELAYS ENERGY EFFICIENCY-LIGHT INDUSTRIAL SAFETY EQUIPMENTS MEGGER MXED-FREQUENCY AC SIGNALS PRINCIPLE OF DIGITAL COMPUTING QUESTIONS REACTANCE AND IMPEDANCE-CAPATIVE SEQUENTIAL CIRCUITS SERRIES-PARALLEL COMBINATION CIRCUITS SHIFT REGISTERS WIRELESS BUILDING SERVICES COMPRESSOR CRANES DIVIDER CIRCUIT AND KIRCHHOFF`S LAW ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS 1 ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS B ELECTRICAL TOOL KIT ELECTRICIAN JOB DESCRIPTION INDUSTRIAL DRIVES LAPTOP SCIENCE THERMOCOUPLE TRIGONOMENTRY REFERENCE UART oscilloscope BIOMASS CONTACTOR ELECTRIC ILLUMINATION ELECTRICAL SAFETY TRAINING ELECTROMECHANICAL FEATURED FILTER DESIGN HARDWARE JUNCTION FIELD-EFFECT TRANSISTORS NASA NUCLEAR POWER VALVE COLOR CODES ELECTRIC TRACTION FLEXIBLE ELECTRONICS FLUKE GEARMOTORS INTRODUCTION LASSER PID PUMP SEAL ELECTRICIAN CAREER ELECTRICITY SUPPLY AND DISTRIBUTION MUSIC NEUTRAL PERIODIC TABLES OF THE ELEMENTS POLYPHASE AC CIRCUITS PROJECTS REATORS SATELLITE STAR DELTA VIBRATION WATERPROOF