(Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO)
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi imejipanga kudhibiti uhalifu unaofanywa na na baadhi watu kwa kupora fedha za wafanyabiashara au watu binafsi kwa kutumia usafiri wa Pikipiki maarufu kama bodaboda.
Akijibu swali la Mhe. Oscar Rwegasira Mukasa Mbunge wa Biharamulo Magharibi (CCM) lililouliza ni zipi takwimu sahihi za matukio ya ujambazi yanayohusiana na uporajiwa fedha,Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Yussuf Massauni amesema matukio ya ujambazi yanayohusisha uporaji wa fedha kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi 2015 kama takwimu zinavyosema , kwa mwaka 2013 matukio 1.266, mwaka 2104 matukio 1,127 na mwaka 2015 yalikuwa 931.
” Jeshi la polisi limechukua hatua kwa kufanya kazi karibu na mabenki nchini ili kubaini kama kuna wafanyakazi wa mabenki wanashirikia na majambazi kufanya uporaji huo na watakaobainika tutawachukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani watakaokamatwa”
“ Napenda kuwaomba wananchi kutupa ushirikiano na hasa kwa wafanyabiashara wanaochukua fedha nyingi ili tuweze kuwapatia ulinzi ili kupunguza, ama kuondoa kabisa vitendo hivi vya uporaji wa fedha vilivyokothiri nchini kwa sasa” Alisema Mhe Massauni.
Aidha amewaomba waheshimiwa Wabunge kutoa elimu kwa wananchi wao kuhusu maswala ya ulinzi na usalama ili kupunguza vitendo vya uhalifu hasa uporaji wa fedha kwa wafanyabiashara kwa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi wakiona tukio lolote linalopangwa kwa ajili ya kupora fedha.
Serikali kupitia Jeshi la Polisi linafanya ukaguzi wa pikipiki zote nchini ili kubaini uhalali wake na uhalali wa wamiliki wake ili kuweza kubaini pikipiki na wamiliki wanaohusika na vitendo vya uporaji wa fedha vinavyoshamiri siku hadi siku
No comments:
Post a Comment