Rais wa
Shilikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT Mutta Rwakatare katikati
akimkabidhi Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila
‘Super D’ mchango uliotolewa na wadau mbalimbali kwa ajili ya lambilambi
ya marehemu Mohamed Chibumbuli kilichotokea juzi Mkoa wa Mtwara Wilaya
ya Masasi kushoto ni katibu Mkuu wa shirikisho hilo Makole Mashaga .
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Ndondi Tanzania (BFT), Makore Mashaga kushoto
akipeana mkono na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu
Mhamila ‘Super D’ baada ya kumkabidhi fedha za lambilambi zilizotolewa
na wadau mbalimbali wakati wa mashindano ya ngumi ya taifa yaliyofanyika
katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe .
Bondia
Selemani Kidunda kushoto akimshambulia Mstafa Mtoro wakati wa mashindano
ya taifa yaliyomalizika katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe
jijini Dar es salaam Kidunda alishinda kwa K.O ya raundi ya kwanza .
Msanii wa
filamu, Shamsa Ford kushoto akipambana na MTANGAZAJI WA TIMES FM,
KHADIJA SHAIBU “DIDA’ wakirushiana makonde wakati wa mashindano ya taifa
ambapo wao walionesha umwamba. (P.T)
Msanii wa
filamu, Shamsa Ford kushoto na MTANGAZAJI WA TIMES FM, KHADIJA SHAIBU
“DIDA’ wakinyoshwa mikono juu baada ya mpambano wao wakati wa
mashindano ya taifa ambapo wao walionesha umwamba
Msanii wa filamu, Shamsa Ford kushoto na MTANGAZAJI WA TIMES FM, KHADIJA SHAIBU “DIDA’
Mjumbe wa
maendeleo ya wanawake BFT Aisha Voniatis akimvisha medali ya dhaabu
bondia Leonard Machichi wakati wa mashindano ya taifa
Mjumbe wa
maendeleo ya wanawake BFT Aisha Voniatis akimvisha medali ya dhaabu kwa
bondia Zulfa Macho kulia ni bondia Halima Ramadhani wa pili kushoto
ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ndondi Tanzania (BFT), Makore Mashaga
Bondia
Ismail Gaitano kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na
Mwalami Salum wakati wa mashindano ya taifa yaliyomalizika katika
viwanja vya Tanganyika Packers Gaitano alishinda mpambano uho.
No comments:
Post a Comment