Mahakama
ya Wilaya ya Manyoni, mkoani Singida, imewahukumu mtu na kaka yake,
kutumikia kifungu cha miaka 20 kila mmoja na kulipa fidia ya sh. milioni
270, baada ya kuwatia hatiani kwa makosa ya kukutwa na meno ya tembo,
silaha na risasi kinyume cha sheria.
Washitakiwa
hao ni Nicodem Mchongareli na Festol Mchongareli, ambao walikuwa
wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 13 ya mwaka jana.
Wanadaiwa
kukutwa na meno ya tembo mawili yenye thamani ya sh. milioni 27,
bunduki tatu zikiwemo za aina ya Riffle, risasi 25 na maganda yake 15.
Hukumu
hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Joyce Minde, baada ya upande wa Jamhuri
uliokuwa ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Salim Msemo na ule wa utetezi
kufunga ushahidi.
Akisoma
hukumu hiyo, Hakimu Joyce alisema wakati wa usikilizwaji wa shauri
hilo, upande wa jamhuri ulileta mashahidi watano na washitakiwa baada ya
kuonekana wana kesi ya kujibu walijitetea wenyewe.
“Mahakama
imewaona washitakiwa hao wana hatia baada ya upande wa Jamhuri
kuthibitisha mashitaka dhidi yao pasi na kuacha shaka yoyote,” alisema.
Hakimu
huyo aliwapa adhabu washitakiwa hao kwa kukutwa na meno ya tembo,
kutumikia kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja na kulipa serikali sh.
milioni 270.
Pia
shitaka la pili wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka miwili jela au
kulipa faini ya sh. milioni 333 na makosa mengine kutumilia kifungo cha
miaka miwili au kulipa faini ya sh. milioni mbili kwa kila shitaka.
Adhabu za vifungo zinakwenda sambamba, hivyo washitakiwa hao watatumikia kifungo cha miaka 20 kila mmoja
No comments:
Post a Comment