Serikali haitokuwa tayari kuwaona watumishi wa umma wachache wakinufaika na kufaidi pesa za walipa kodi hususan wa kipatao cha chini na wale maskini
Hayo yamesema wilayani Nzega na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kigwangwalla alipokuwa akiwahutubia wananchi wa wilaya hiyo
Dkt.Kigwangwalla alisema serikali ya awamu ya tano inawataka watumishi wote nchini kufanya kazi za kuwahudumia wananchi na kuacha uzembe kwani awamu hii haiwezi kuwavumilia watumishi wa namna hiyo.
“Serikali haitowavumilia watumishi wazembe,hivyo tutaendelea kuwafungia mageti na kuwashughulikia wale wazembe,tunataka watumishi wa umma wafanye kazi ya kuwahudumia wananchi kwa ufanisi,mtumishi akizembea tutamtumbua majipu,akichelewa tunamfungia geti na akiiba tunamfilisi pamoja na kumpeleka jela,hii ndiyo serikali ya hapa kazi tu”
Aidha alisema serikali ya awamu ya tano inataka kero za wananchi zifanyiwe kazi na kutekeleza ahadi zote za ilani ya uchaguzi ya ccm zinatimizwa.
“hatutomuonea mtu,lakini tutafanyia kazi pale penye matatizo.Tunataka Tanzania mpya ya mwaka 2015 ,hatutaki hadithi wala ahadi”
Hata hivyo aliwataka wazazi wote wenye watoto wenye umri wa kwenda shule kuwapeleka watoto wao kuanza masomo kwani elimu kwa sasa ni bure na hakuna michango yoyote.
“Natoa wito kwa walimu wote wasitoze michango yeyote wala ushuru kwa wazazi wanaowapeleka kuwaandikisha watoto shule kwani shule zimepatiwa pesa za kuendeshea shule hizo."
Dkt. Kigwangwalla aliwakumbusha watumishi wa umma kujipanga na kama watagundulika ni majipu hawatosita kuwatumbua hadi kina kitoke usaha na damu bila huruma
No comments:
Post a Comment