Msafara
wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukikatisha misitu na
mabonde wakati ukielekea kata ya Mwangeza kijiji cha Kibampa ambako
jamii hiyo inaishi.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia Sola zinazosukuma maji
kwenye kisima cha mradi wa maji yanayotumika kwenye kijiji pamoja na
shule ya msingi ya Munguli iliyopo wilaya ya Mkalama mkoani Singida.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya mradi wa maji
wa kijiji cha Munguli kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Ndugu
Christopher Ngubiagai.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ndani ya hosteli ya shule ya
msingi Munguli ambayo wanasoma watoto wa Kihadzabe.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakulima wakati
akiwa njiani kuelekea kata ya Mwangeza kijiji cha Kibampa.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakulima wakati
akiwa njiani kuelekea kata ya Mwangeza kijiji cha Kibampa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikaribishwa kijiji cha Kibampa na wakazi wa hapo amabao ni Wahadzabe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akifurahia jambo na kijana wa kabila la Kihadzabe
Wahadzabe wakiwa kwenye kikao maalum kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakishiriki kupanda mihogo kwenye
shamba ya la Wahadzabe kwenye kijiji cha Kibampa wilaya ya Mkalama.
Mkuu
wa Wilaya ya Mkalama Ndugu Christopher Ngubiagai akimuelekeza Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana namna Wahadzabe wanavyosaga mtama
kwa kutumia jiwe.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana leo ameweka historia ya kuwa
kiongozi wa nne mkubwa wa Kitaifa kufika kwenye kijiji cha Munguli na
Kibampa ambavyo wanaishi jamii ya Wahadzabe .Kijiji cha Munguli
kilitembelewa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere,
akifuatiwa na aliyekuwa Makamu wake Abdu Jumbe na Mama Sofia Kawawa.
Jamii ya Wahadzabe inaishi kwa kutegemea uwindaji,kula matunda ya
porini,mizizi ,wadudu na miti hata hivyo juhudi kubwa zimefanyika kuanza
kuwafundisha kilimo, kuwapeleka watoto shule ,zaidi ya Wahadzabe 305
wanasoma kwenye shule ya msingi Munguli, pamoja na vijana zaidi ya 50
kupelekwa kujiunga na JKT.
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone kwa jitihada zake
za kuwasaidia jamii ya Wahadzabe ikiwa pamoja na kuhakikisha wanapata
elimu, wanajifunza kilimo lakini pia uamuzi wa kupima maeneo ya
Wahadzabe ili wamiliki ardhi yao wenyewe.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akiwa kwenye nyumba
maalum ya chifu wa wahadzabe pamoja na Mwenyekiti wa Wahadzabe Edward
Mashimba na Mama Sarah Philipo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakitoka kwenye nyumba ya Chifu wa
Wahadzabe iliyopo kijiji cha Kibampa kata ya Mwangeza wilaya ya Mkalama
mkoani Singida
wakazi
wa kijiji cha Kibampa ambaco wakazi wake ni jamii ndogo yenye kaya 300
ya Wahadzabe wakishangilia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana
alipokuwa akiwahutubia
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha
Kibampa ambako wakazi wake ni jamii ndogo yenye kaya 300 ya
Wahadzabe,kushoto ni Mwenyekiti wa Wahadzabe Ndugu Edward Mashimba
(kushoto) ambaye alikuwa akitafsiri kwa lugha ya Kihadzabe
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha
Kibampa ambako wakazi wake ni jamii ndogo yenye kaya 300 ya
Wahadzabe,kushoto ni Mwenyekiti wa Wahadzabe Ndugu Edward Mashimba
(kushoto) ambaye alikuwa akitafsiri kwa lugha ya Kihadzabe
No comments:
Post a Comment