Jecha Adai Maalim Seif Ni Mgombea Halali Na ZEC Haitambui Kujitoa KwakeMwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, ameibuka tena na kutangaza kukamilika kwa matayarisho ya uchaguzi wa marejeo Machi 20, mwaka huu huku akikataa kutoa majina ya wagombea.

Jecha ambaye tangu afute uchaguzi alionekana hadharani Januari 12, 2016 wakati wa sherehe za Mapinduzi na baadaye kwenye televisheni akitangaza tarehe ya uchaguzi huo wa marudio, alisema wagombea wote ‘waliojitoa’ watapewa haki zote wanazostahiki kupewa kama wagombea kwa kuwa hawakufuata taratibu za kisheria za tume hiyo akimaanisha kuwa hakuna mgombea aliyejitoa kauli ambayo inapingana na msimamo wa CUF ambayo imetangaza kuwa mgombea wake wa urais Maalim Seif Sharif Hamad hatagombea.

Kama alivyofanya wakati anatangaza tarehe ya uchaguzi wa marudio, jana alizungumza kupitia mwandishi wa Televisheni ya Taifa (TBC), akiwaacha waandishi waliokuwa wameitwa kwa ajili ya mkutano wake nje ya ofisi hiyo.

Jecha ambaye amekuwa haonekani hadharani isipokuwa katika matukio machache, alisema tume yake inawahesabu waliokuwa wagombea katika uchaguzi ulio futwa kuwa ni halali, licha ya kuandika barua za kujitoa katika tume hiyo. 

“Pamoja na kuwa wagombea wengi, hasa wa CUF, kuandika barua za kujitoa katika ofisi za ZEC wilaya na makao makuu, hakuna barua hata moja ambayo imefuata utaratibu wa kisheria na kwa mantiki hiyo, bado tunahesabu wagombea hao ni halali katika uchaguzi mkuu wa marejeo,”alisema Jecha. 

Katika taarifa hiyo, Jecha alisema vyama vinane vimeshathibitisha ushiriki wake katika uchaguzi huo vikiwamo Tadea, ACT, ADC, AFP, SAU, TLP na CCM na utaratibu wa kuwapatia ulinzi wagombea hao umeshaanza. 

Jecha alisema ofisi yake imeshafanya mawasiliano na vyama na wagombea na kuwapa taarifa mbalimbali za matayarisho ya uchaguzi, ili waanze taratibu za kupanga mawakala wao.

Alisema baadhi ya vyama vimetoa taarifa kupitia vyombo vya habari kuwa havitashiriki katika uchaguzi, na kuwataka wagombea wao kuandika barua za kutoshiriki katika upigaji kura huo.

“Swala hili naomba nilitolee ufafanuzi kidogo kwa kuwa kauli za vyama hivyo zimewachanganya baadhi ya wagombea waliodhaminiwa na vyama hivyo, ambao bado wanataka kugombea katika uchaguzi huo,”alisema Jecha.

Alisema kila chama cha siasa kilichosajiliwa kinachokusudia kushiriki uchaguzi wa Rais kitawasilisha jina la mgombea wake wa urais kwa tume, na ili mtu awe ameteuliwa kihalali kuwa mgombea urais ni lazima awe amedhaminiwa kwa maandishi na watu wasiopungua 200 ambao wameandikishwa kuwa wapiga kura kutoka kila mkoa wa Zanzibar.

“Kwa bahati mbaya mpaka tunapowasilisha taarifa hii, hakuna chama hata kimoja kati ya vyama ambavyo vimejinadi kuwa havitashiriki katika uchaguzi kilichoiandikia Tume kuwa kimefuta udhamini wa wagombea wake kushiriki katika uchaguzi,” alisema Jecha katika taarifa yake.

“La pili ni kuwa utaratibu wa kujitoa kwa wagombea katika uchaguzi umefafanuliwa vizuri sana katika kanuni ya uchaguzi ya mwaka 2015,”alisema mwenyekiti huyo akisisitiza kuwa haukufuatwa.

Kwa mujibu wa vifungu hivyo, alisema mgombea wa urais anaweza kujiondoa kwa kutoa taarifa ya maandishi aliyoitia saini mwenyewe atakayoiwasilisha kwa mwenyekiti si zaidi ya saa 10 jioni siku ya uteuzi.

“Mgombea uwakilishi na udiwani anaweza kujiondoa kwa kutoa taarifa ya maandishi aliyoitia saini mwenyewe atakayoiwasilisha kwa msimamizi wa uchaguzi si zaidi ya saa 10 jioni ya siku inayofuatia siku ya uteuzi."

Jecha alifafanua kuwa tarifa ya kujiondoa chini ya kanuni hizo inatakiwa iambatanishwe na tamko la kisheria lililotolewa na kutiwa saini na mgombeya mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu kwa mgombea wa urais na hakimu kwa mgombea wa uwakilishi au udiwani, mambo ambayo hayakufanyika.

Kuhusu daftari la wapigakura, Jecha alisema kazi ya uchapishaji wa madaftari na vituo vya kupigia kura ndani na nje imeshakamilika, na wanatarajia mwisho wa mwezi huu majina hayo kubandikwa.

Alisema ratiba ya mafunzo kwa wasaidizi na wasimamizi wa majimbo imeshakamilika, na mafunzo hayo kwa Unguja na Pemba yataendeshwa Februari 22-28 na wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo watapewa mafunzo Machi 2 hadi Machi 5.

Alisema mafunzo mengine yatakayotolewa ni ya wasaidizi wa vituo vya kupigia kuwa ambayo yamepangwa kufanyika Machi 11 -13 na mafunzo ya mawakala wa uchaguzi siku ya Machi 14 na mafunzo ya walinzi wa vituo vya kupigia kura Machi 15, 2016.

Jecha alisema kazi ya upangaji wa vifaa vya kupigia kura kwa ajili ya kusambazwa wilayani tayari imeanza katika ghala za ZEC za Unguja na Pemba na baada ya kukamilika kwa kazi hiyo, utaratibu wa kuvisafirisha katika wilaya husika utaandaliwa.

Kuhusu uchapishaji karatasi za kura, mwenyekiti huyo alisema matayarisho yamekamilika baada ya tume kumpitisha mchapishaji wa karatasi hizo.
Previous
Next Post »
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Label

KITAIFA NEWS KIMATAIFA MICHEZO BURUDANI SIASA TECHNICAL ARTICLES f HAPA KAZI TU. LEKULE TV EDITORIALS ARTICLES DC DIGITAL ROBOTICS SEMICONDUCTORS MAKALA GENERATOR GALLERY AC EXPERIMENTS MANUFACTURING-ENGINEERING MAGAZETI REFERENCE IOT FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY ELECTRONICS ELECTRICAL ENGINEER MEASUREMENT VIDEO ZANZIBAR YETU TRANSDUCER & SENSOR MITINDO ARDUINO RENEWABLE ENERGY AUTOMOBILE SYNCHRONOUS GENERATOR ELECTRICAL DISTRIBUTION CABLES DIGITAL ELECTRONICS AUTOMOTIVE PROTECTION SOLAR TEARDOWN DIODE AND CIRCUITS BASIC ELECTRICAL ELECTRONICS MOTOR SWITCHES CIRCUIT BREAKERS MICROCONTROLLER CIRCUITS THEORY PANEL BUILDING ELECTRONICS DEVICES MIRACLES SWITCHGEAR ANALOG MOBILE DEVICES CAMERA TECHNOLOGY GENERATION WEARABLES BATTERIES COMMUNICATION FREE CIRCUITS INDUSTRIAL AUTOMATION SPECIAL MACHINES ELECTRICAL SAFETY ENERGY EFFIDIENCY-BUILDING DRONE NUCLEAR ENERGY CONTROL SYSTEM FILTER`S SMATRPHONE BIOGAS POWER TANZIA BELT CONVEYOR MATERIAL HANDLING RELAY ELECTRICAL INSTRUMENTS PLC`S TRANSFORMER AC CIRCUITS CIRCUIT SCHEMATIC SYMBOLS DDISCRETE SEMICONDUCTOR CIRCUITS WIND POWER C.B DEVICES DC CIRCUITS DIODES AND RECTIFIERS FUSE SPECIAL TRANSFORMER THERMAL POWER PLANT cartoon CELL CHEMISTRY EARTHING SYSTEM ELECTRIC LAMP ENERGY SOURCE FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 2 BIPOLAR JUNCTION TRANSISTOR 555 TIMER CIRCUITS AUTOCAD C PROGRAMMING HYDRO POWER LOGIC GATES OPERATIONAL AMPLIFIER`S SOLID-STATE DEVICE THEORRY DEFECE & MILITARY FLUORESCENT LAMP HOME AUTOMATION INDUSTRIAL ROBOTICS ANDROID COMPUTER ELECTRICAL DRIVES GROUNDING SYSTEM BLUETOOTH CALCULUS REFERENCE DC METERING CIRCUITS DC NETWORK ANALYSIS ELECTRICAL SAFETY TIPS ELECTRICIAN SCHOOL ELECTRON TUBES FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 1 INDUCTION MACHINES INSULATIONS ALGEBRA REFERENCE HMI[Human Interface Machines] INDUCTION MOTOR KARNAUGH MAPPING USEUL EQUIATIONS AND CONVERSION FACTOR ANALOG INTEGRATED CIRCUITS BASIC CONCEPTS AND TEST EQUIPMENTS DIGITAL COMMUNICATION DIGITAL-ANALOG CONVERSION ELECTRICAL SOFTWARE GAS TURBINE ILLUMINATION OHM`S LAW POWER ELECTRONICS THYRISTOR USB AUDIO BOOLEAN ALGEBRA DIGITAL INTEGRATED CIRCUITS FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 3 PHYSICS OF CONDUCTORS AND INSULATORS SPECIAL MOTOR STEAM POWER PLANTS TESTING TRANSMISION LINE C-BISCUIT CAPACITORS COMBINATION LOGIC FUNCTION COMPLEX NUMBERS ELECTRICAL LAWS HMI[HUMANI INTERFACE MACHINES INVERTER LADDER DIAGRAM MULTIVIBRATORS RC AND L/R TIME CONSTANTS SCADA SERIES AND PARALLEL CIRCUITS USING THE SPICE CIRCUIT SIMULATION PROGRAM AMPLIFIERS AND ACTIVE DEVICES BASIC CONCEPTS OF ELECTRICITY CONDUCTOR AND INSULATORS TABLES CONDUITS FITTING AND SUPPORTS CONTROL MOTION ELECTRICAL INSTRUMENTATION SIGNALS ELECTRICAL TOOLS INDUCTORS LiDAR MAGNETISM AND ELECTROMAGNETISM PLYPHASE AC CIRCUITS RECLOSER SAFE LIVING WITH GAS AND LPG SAFETY CLOTHING STEPPER MOTOR SYNCHRONOUS MOTOR AC METRING CIRCUITS APPS & SOFTWARE BASIC AC THEORY BECOME AN ELECTRICIAN BINARY ARITHMETIC BUSHING DIGITAL STORAGE MEMROY ELECTRICIAN JOBS HEAT ENGINES HOME THEATER INPECTIONS LIGHT SABER MOSFET NUMERATION SYSTEM POWER FACTORS REACTANCE AND IMPEDANCE INDUCTIVE RESONANCE SCIENTIFIC NOTATION AND METRIC PREFIXES SULFURIC ACID TROUBLESHOOTING TROUBLESHOOTING-THEORY & PRACTICE 12C BUS APPLE BATTERIES AND POWER SYSTEMS ELECTROMECHANICAL RELAYS ENERGY EFFICIENCY-LIGHT INDUSTRIAL SAFETY EQUIPMENTS MEGGER MXED-FREQUENCY AC SIGNALS PRINCIPLE OF DIGITAL COMPUTING QUESTIONS REACTANCE AND IMPEDANCE-CAPATIVE RECTIFIER AND CONVERTERS SEQUENTIAL CIRCUITS SERRIES-PARALLEL COMBINATION CIRCUITS SHIFT REGISTERS BUILDING SERVICES COMPRESSOR CRANES DC MOTOR DRIVES DIVIDER CIRCUIT AND KIRCHHOFF`S LAW ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS 1 ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS B ELECTRICAL TOOL KIT ELECTRICIAN JOB DESCRIPTION LAPTOP THERMOCOUPLE TRIGONOMENTRY REFERENCE UART WIRELESS BIOMASS CONTACTOR ELECTRIC ILLUMINATION ELECTRICAL SAFETY TRAINING FILTER DESIGN HARDWARE INDUSTRIAL DRIVES JUNCTION FIELD-EFFECT TRANSISTORS NASA NUCLEAR POWER SCIENCE VALVE WWE oscilloscope 3D TECHNOLOGIES COLOR CODES ELECTRIC TRACTION FEATURED FLEXIBLE ELECTRONICS FLUKE GEARMOTORS INTRODUCTION LASSER MATERIAL PID PUMP SEAL ELECTRICIAN CAREER ELECTRICITY SUPPLY AND DISTRIBUTION MUSIC NEUTRAL PERIODIC TABLES OF THE ELEMENTS POLYPHASE AC CIRCUITS PROJECTS REATORS SATELLITE STAR DELTA VIBRATION WATERPROOF