January Makamba Awapa Makavu Wapinzani - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Friday, 5 February 2016

January Makamba Awapa Makavu WapinzaniWaziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, amewataka baadhi ya wabunge wa upinzani kuwa na lugha nzuri dhidi ya serikali ili waweze kupata ushirikiano mzuri na viongozi hao pamoja na serikali.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira na Muungano) Mh. January Makamba amefunguka na kusema kuwa wao kama Chama cha Mapinduzi ndiyo wenye dola na wao ndiyo wanaongoza serikali hivyo amewataka baadhi ya wabunge wa upinzani kuwa na lugha nzuri dhidi ya serikali ili waweze kupata ushirikiano mzuri na viongozi hao pamoja na serikali hiyo pindi watakapo hitaji msaada wowote kutoka serikalini.

January Makamba amesema hayo bungeni na kudai amefadhaishwa na michango ya wabunge wa upinzani ambao walikuwa wakitumia lugha za kuudhi dhidi ya Rais pamoja na viongozi wa serikali.

"Najua kazi ya upinzani ni kulaumu hivi nyinyi wapinzani kwa kazi anayofanya Rais Magufuli leo mngepewa nafasi wapinzani ni kipi ambacho mngefanya zaidi ya hiki? "Alihoji January Makamba

Lakini katika hatua nyingine amesema aina ya uchangiaji nyingine ya wabunge bungeni ni kama walikuwa wakiwatisha watanzania juu ya sakata la Zanzibar na alimaliza kwa kusema kuwa utatuzi wa suala la Zanzibar haupatikani barabarani, haupatikani bungeni bali unapatikana katika Katiba na sheria za Zanzibar pekee na si kitu kingine.
Post a Comment