Jaji Mkuu Wa Kenya Ataka Mazungumzo Yaendelee Kumaliza Mzozo Zanzibar - LEKULE

Breaking

4 Feb 2016

Jaji Mkuu Wa Kenya Ataka Mazungumzo Yaendelee Kumaliza Mzozo Zanzibar


Jaji Mkuu wa Kenya Dk Willy Mutunga ameshauri kuendelea na mazungumzo ya kutafuta suluhu ya kisiasa Zanzibar kwa lengo la kuimarisha Muungano wa Tanzania, huku akionesha hofu kuwa ukivunjika unaweza kuwa na athari kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Jaji Mutunga alitoa ushauri huo jana wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Mahakama Kuu Dar es Salaam.

“Tanzania ina kila cha kujivunia kwani hakuna ukabila, wanajivunia lugha yao, utamaduni na msimamo wa ujamaa. Sidhani kama mmeingia katika ubepari na ukabaila,’’
 alisema Jaji huyo na kuongeza kuwa msimamo wa Mwalimu Julius Nyerere ulijali maslahi ya wengine katika masuala mbalimbali ikiwemo uchumi na siasa.

Aidha, alisema Tanzania inafanya vizuri kuliko Kenya katika masuala ya usikilizaji wa kesi. Alisema watajifunza namna ya kusikiliza kesi haraka ili kumaliza mashauri kwa muda.

“Kenya iliwahi kusikiliza kesi tatu kwa zaidi ya miaka 33 hivyo ni tofauti na wanavyofanya wenzetu Watanzania,’’ alisema Jaji Mutunga na kusisitiza kuwa katika Afrika Mashariki, majaji na mahakimu wengi hawachukui rushwa na kwamba njia nzuri ni kuwatoa wanaopokea rushwa.

No comments: