Hello

Welcome lekule blog

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation.
together in the world. #lekule86
Join us on

Jaji Mihayo Amtetea Rais Magufuli........ Asema Sio Dikteta na Kauli Yake Kuhusu Mahakama Ilikuwa Ni Kuwataka Majaji Wafanye Kazi Kwa BidiiSiku tatu baada ya Rais John Magufuli kueleza kuwa yeye si kichaa, si dikteta wala mnyama, Jaji Thomas Mihayo ameungana na mkuu huyo wa nchi akisema hajauona udikteta wake.

Jaji Mihayo alikuwa akifafanua kauli alizotoa Rais Magufuli kwenye kilele cha Siku ya Sheria, wakati alipomuahidi Jaji Mkuu Othman Chande Sh12.3 bilioni za kuendeshea shughuli za mahakama na kumtaka aharakishe kushughulikia kesi za ufisadi ili Serikali iokoe Sh1 trilioni, ambazo kati ya hizo atatoa Sh250 bilioni kwa ajili ya Idara ya Mahakama.

Rais pia alitaka kesi ambazo watuhumiwa wanakamatwa na ushahidi, zifikishwe mahakamani mara moja na kuamuliwa, lakini akataka asichukuliwe kuwa ni dikteta kutokana na maamuzi yake.

“Ninapochukua hatua mimi si mnyama, si dikteta, si shetani. Ni mpole kweli, lakini inafika mahali lazima nifanye (uamuzi). Yanayofanyika serikalini ni mambo ya ajabu sana, nataka kutoa sadaka yangu, inawezekana hata nikifa naweza kuwa rais wa malaika,” alisema.

Kauli hiyo imeibua mjadala miongoni mwa wanasheria wanaodai Rais anaingilia uhuru wa mahakama kwa kutaka uamuzi wa kesi hizo ufanywe kwa utashi wa Serikali, huku baadhi ya hatua kali anazochukua zikielezewa kuwa zina harufu ya udikteta. 

Lakini jana, mkuu huyo wa nchi alipata mtetezi wakati Jaji Mihayo alipoongea na waandishi kufafanua kauli hiyo ya Siku ya She ria, akisema Rais dikteta ni yule asiyefuata misingi ya sheria.

“Wanaosema Magufuli ni dikteta hawawajui madikteta. Hakuna kiongozi dikteta Afrika Mashariki isipokuwa Idi Amini tu,” alisema jaji huyo mstaafu ambaye alisema ameamua kutoa ufafanuzi huo baada ya kuona mjadala mkubwa kuhusu kauli hiyo ya Rais na kupata baraka kutoka kwa Jaji Mkuu, Othuman Chande.

Jaji Mihayo, ambaye ni mwenyekiti wa majaji wastaafu, alihoji inawezekanaje kiongozi ambaye mataifa mengine wanatamani akaongoze nchi yao angalau kwa miezi miwili, aonekane kuwa ni dikteta.

“Magufuli anafuata sheria kwa sababu hajafanya jambo lolote ambalo linamfanya awe juu ya sheria. Sijawahi kusikia kasema mfunge huyu au kusema sheria hii isitumike na hii itumike” alisema.

Alisema ni kawaida kwa viongozi wanaokemea uovu kuonekana kama madikteta kwa sababu wanataka kuondoa rushwa.

Kadhalika, Jaji Mihayo alisema anaupenda utendaji kazi wa Magufuli ili wanaokiuka sheria wawajibishwe na walalahoi wapate haki yao.

Magufuli na Mahakama 
Kuhusu ahadi yake ya kuipa Idara ya Mahakama Sh12.3 bilioni ili izitumie kwenye shughuli zake na agizo la kuharakisha uamuzi wa kesi 442 ili Serikali iokoe Sh1 trilioni, Jaji Mihayo alisema kitendo hicho hakiingilii uhuru wa mahakama bali ni katika kuhakikisha kesi zinamalizwa kwa wakati na serikali inakusanya mapato ya kutosha.

“Maneno ya Rais ya kuwataka majaji wamalize kesi kwa haraka na kuwaahidi kiasi kile cha fedha, si kuwahonga bali ni motisha na mbinu ya kukusanya mapato,” alisema.

Alisema kauli ya Rais isitafisriwe kuwa ni lazima Serikali ishinde kesi dhidi ya rufaa ya kodi, bali alitaka majaji wafanye kazi zao kwa wepesi zaidi.

Akifafanua kesi za rufaa za kodi, Jaji Mihayo alisema mashauri hayo yatakusanya fedha nyingi kwa hata kama wanaodaiwa watashinda, kisheria ni lazima watoe theluthi ya kodi wanayodaiwa.

Jaji Mihayo pia alisema maneno ya Magufuli yasichukuliwe kuwa yatawavuruga majaji kwa sababu wanafanya kazi yao kwa kufuata kanuni na sheria.

“Uhuru wa mahakama upo ‘guaranteed (umehakikishwa)’ na katika kifungu namba 107 (a) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano.Hata kama Rais akiamrisha vipi, kama ni kitu ambacho ni kinyume na utaratibu, hakiwezi kutekelezwa” alisema.

Kuhusu Magufuli kuwachukulia hatua majaji na mahakimu 502 ambao hawajafikia malengo ya kumaliza kati ya kesi 250 na 260 kwa mwaka, Jaji Mihayo alisema JPM alionyesha kukerwa na ucheleweshaji wa kesi na wala si kuingilia uhuru wa mahakama.

Alisema hata Jaji Mkuu Othman Chande alishachukua hatua kwa kuwataka mahakimu hao watoe maelezo kabla sheria haijachukua mkondo wake.

“Tatizo la ucheleweshaji wa kesi ni kubwa, si dogo kama unavyofikiria ndiyo maana linamkera JPM,” alisema.

Utendaji wa mawaziri, wakuu wa mikoa 
Kadhalika Jaji Mihayo pia alizungumzia pia jinsi mawaziri wa JPM wanavyotoa kauli za kuwafukuza kazi au kuwasimamisha watendaji wa Serikali, akisema siasa inatawala kuliko sheria.

Alisema kisheria kiongozi wa Serikali hawezi kusimamishwa kazi au kufukuzwa bila maandishi.

“Watendaji hawatachukuliwa hatua bila kauli ya waziri kuwa katika maandishi, hilo jambo halichukuliwi kijumla tu,” alisema.

Alisema Katibu Mkuu Kiongozi akimsimamisha au kumfukuza mtu kazi, hilo linakuwa limeshafanyiwa kazi kwa kina.

“Vinginevyo, huwezi kumfukuza mtu kazi bila mchakato na uchunguzi wa kuhakiki kama ni kweli ana haki ya kusimamishwa au kufukuzwa,”alisema.

Share this:

ABOUTME

Hi all. This is deepak from Bthemez. We're providing content for Bold site and we’ve been in internet, social media and affiliate for too long time and its my profession. We are web designer & developer living India! What can I say, we are the best..

Post a Comment
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.

Labels

LEKULE TV EDITORIALS ARTICLES DC ROBOTICS DIGITAL SEMICONDUCTORS GENERATOR AC EXPERIMENTS MANUFACTURING-ENGINEERING REFERENCE FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY ELECTRONICS ELECTRICAL ENGINEER MEASUREMENT TRANSDUCER & SENSOR VIDEO ARDUINO RENEWABLE ENERGY AUTOMOBILE TEARDOWN SYNCHRONOUS GENERATOR DIGITAL ELECTRONICS ELECTRICAL DISTRIBUTION CABLES AUTOMOTIVE MICROCONTROLLER SOLAR PROTECTION DIODE AND CIRCUITS BASIC ELECTRICAL ELECTRONICS MOTOR SWITCHES CIRCUIT BREAKERS CIRCUITS THEORY PANEL BUILDING ELECTRONICS DEVICES MIRACLES SWITCHGEAR ANALOG MOBILE DEVICES WEARABLES CAMERA TECHNOLOGY COMMUNICATION GENERATION BATTERIES FREE CIRCUITS INDUSTRIAL AUTOMATION SPECIAL MACHINES ELECTRICAL SAFETY ENERGY EFFIDIENCY-BUILDING DRONE CONTROL SYSTEM NUCLEAR ENERGY SMATRPHONE FILTER`S POWER BIOGAS BELT CONVEYOR MATERIAL HANDLING RELAY ELECTRICAL INSTRUMENTS ENERGY SOURCE PLC`S TRANSFORMER AC CIRCUITS CIRCUIT SCHEMATIC SYMBOLS DDISCRETE SEMICONDUCTOR CIRCUITS WIND POWER C.B DEVICES DC CIRCUITS DIODES AND RECTIFIERS FUSE SPECIAL TRANSFORMER THERMAL POWER PLANT CELL CHEMISTRY EARTHING SYSTEM ELECTRIC LAMP FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 2 BIPOLAR JUNCTION TRANSISTOR 555 TIMER CIRCUITS AUTOCAD BLUETOOTH C PROGRAMMING HOME AUTOMATION HYDRO POWER LOGIC GATES OPERATIONAL AMPLIFIER`S SOLID-STATE DEVICE THEORRY COMPUTER DEFECE & MILITARY FLUORESCENT LAMP INDUSTRIAL ROBOTICS ANDROID ELECTRICAL DRIVES GROUNDING SYSTEM CALCULUS REFERENCE DC METERING CIRCUITS DC NETWORK ANALYSIS ELECTRICAL SAFETY TIPS ELECTRICIAN SCHOOL ELECTRON TUBES FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 1 INDUCTION MACHINES INSULATIONS USB ALGEBRA REFERENCE HMI[Human Interface Machines] INDUCTION MOTOR KARNAUGH MAPPING USEUL EQUIATIONS AND CONVERSION FACTOR ANALOG INTEGRATED CIRCUITS BASIC CONCEPTS AND TEST EQUIPMENTS DIGITAL COMMUNICATION DIGITAL-ANALOG CONVERSION ELECTRICAL SOFTWARE GAS TURBINE ILLUMINATION OHM`S LAW POWER ELECTRONICS THYRISTOR BOOLEAN ALGEBRA DIGITAL INTEGRATED CIRCUITS FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 3 PHYSICS OF CONDUCTORS AND INSULATORS SPECIAL MOTOR STEAM POWER PLANTS TESTING TRANSMISION LINE C-BISCUIT CAPACITORS COMBINATION LOGIC FUNCTION COMPLEX NUMBERS CONTROL MOTION ELECTRICAL LAWS INVERTER LADDER DIAGRAM MULTIVIBRATORS RC AND L/R TIME CONSTANTS SCADA SERIES AND PARALLEL CIRCUITS USING THE SPICE CIRCUIT SIMULATION PROGRAM AMPLIFIERS AND ACTIVE DEVICES APPS & SOFTWARE BASIC CONCEPTS OF ELECTRICITY CONDUCTOR AND INSULATORS TABLES CONDUITS FITTING AND SUPPORTS ELECTRICAL INSTRUMENTATION SIGNALS ELECTRICAL TOOLS INDUCTORS LiDAR MAGNETISM AND ELECTROMAGNETISM PLYPHASE AC CIRCUITS RECLOSER SAFE LIVING WITH GAS AND LPG SAFETY CLOTHING STEPPER MOTOR SYNCHRONOUS MOTOR AC METRING CIRCUITS BECOME AN ELECTRICIAN BINARY ARITHMETIC BUSHING DIGITAL STORAGE MEMROY ELECTRICIAN JOBS HEAT ENGINES HOME THEATER INPECTIONS LIGHT SABER MOSFET NUMERATION SYSTEM POWER FACTORS REACTANCE AND IMPEDANCE INDUCTIVE RECTIFIER AND CONVERTERS RESONANCE SCIENTIFIC NOTATION AND METRIC PREFIXES SULFURIC ACID TROUBLESHOOTING TROUBLESHOOTING-THEORY & PRACTICE 12C BUS APPLE BATTERIES AND POWER SYSTEMS DC MOTOR DRIVES ELECTROMECHANICAL RELAYS ENERGY EFFICIENCY-LIGHT INDUSTRIAL SAFETY EQUIPMENTS MEGGER MXED-FREQUENCY AC SIGNALS PRINCIPLE OF DIGITAL COMPUTING QUESTIONS REACTANCE AND IMPEDANCE-CAPATIVE SEQUENTIAL CIRCUITS SERRIES-PARALLEL COMBINATION CIRCUITS SHIFT REGISTERS WIRELESS BUILDING SERVICES COMPRESSOR CRANES DIVIDER CIRCUIT AND KIRCHHOFF`S LAW ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS 1 ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS B ELECTRICAL TOOL KIT ELECTRICIAN JOB DESCRIPTION INDUSTRIAL DRIVES LAPTOP SCIENCE THERMOCOUPLE TRIGONOMENTRY REFERENCE UART oscilloscope BIOMASS CONTACTOR ELECTRIC ILLUMINATION ELECTRICAL SAFETY TRAINING ELECTROMECHANICAL FEATURED FILTER DESIGN HARDWARE JUNCTION FIELD-EFFECT TRANSISTORS NASA NUCLEAR POWER VALVE COLOR CODES ELECTRIC TRACTION FLEXIBLE ELECTRONICS FLUKE GEARMOTORS INTRODUCTION LASSER PID PUMP SEAL ELECTRICIAN CAREER ELECTRICITY SUPPLY AND DISTRIBUTION MUSIC NEUTRAL PERIODIC TABLES OF THE ELEMENTS POLYPHASE AC CIRCUITS PROJECTS REATORS SATELLITE STAR DELTA VIBRATION WATERPROOF