Idadi ya watu Japan yapungua kwa milioni moja - LEKULE

Breaking

27 Feb 2016

Idadi ya watu Japan yapungua kwa milioni moja

Takwimu rasmi ya idadi ya watu nchini Japan, imeashiria kuwa idadi ya watu nchini humo ilipungua kwa takriban watu milioni moja katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Hii ni mara ya kwanza kwa idadi ya watu nchini humo kushuka tangu mwaka wa 1920, licha ya kuwa wataalamu walikuwa wamebashiri kutokea kwa hali hiyo miongo kadhaa iliyopita, wakisema kuwa kupungua kwa idadi ya watoto wanaozaliwa na kutokuwepo kwa watu wanaoingia nchini humo kuishi.
Tatizo hilo linatarajiwa kuwa mbale zaidi, utafiti uliofanywa na taasisi inayohusika na masuala ya sensa , umebainisha kuwa asilimia arobaini ya raia wa Japan watakuwa na umri wa miaka sitini na tano au zaidi ifikiapo mwaka wa 2050, na hivyo kuzua wasi wasi kuwa gharama ya kuwatunza watu wakongwe nchini humo itapanda zaidi.

No comments: