DKT. KIGWANGALLA ATEMBELEA KAMBI YA WAGONJWA WA KIPINDUPINDU, IRINGA - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Tuesday, 16 February 2016

DKT. KIGWANGALLA ATEMBELEA KAMBI YA WAGONJWA WA KIPINDUPINDU, IRINGA

dk-kigwanomic-1
dk-kigwanomic-1Naibu Waziri wa Afya, .Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla leo amewatembele wahanga wa ugonjwa wa kipindupindu mkoani Iringa na kuwaeleza kuwa wasiwe na wasiwasi serikali ipo pamoja nao na inafanya jitihada kuokoa maisha yao.
Pia alieleza kwa sasa serkali inashughulikia uokoaji wa maisha na inashughulikia suala la chakula na malazi na kwamba wananchi wanatakiwa kunawa mikono vizuri ili kujiepusha na ugonjwa huo, ambao umesababishwa na mafuriko ya mto Ruaha kutokana na maji kujaa na kuacha njia yake.
Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Dkt. Ignas Mlowe alisema maji hayo yalisomba nyumba na kubomoa vyoo.
Kuafuatia hali ya mafuriko Dkt. Kigwangalla aliamuru chopa iliyompeleka katika tukio itumike kuwaokoa wakina mama wanne mmoja kati yao ni mjamzito na watoto wanne mmoja wa mchanga wa wiki mmoja.
Alisema ameridhishwa na huduma za uokoaji hivyo aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa waokoaji ili kutolifanya zoezi kuwa gumu.
Aliwasisitiza wananchi hao kunywa maji kwa wingi kwani ni muhimu kwa maisha yao pia alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kassela kuhakikisha wananchi wanakuwa na vyoo na kufukia madimbwi ya machafu ili kujiepusha na ugonjwa huo.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alisema ugonjwa huo umeathiri watu 223 na kuua mtu mmoja pia wagonjwa waliolazwa kambini ni 40.
Post a Comment